UJERUMANI-WAKIMBIZI-USALAMA-HAKI

Wakimbizi waendelea kuingia Ujerumani kwa wingi

Wakimbizi wanafanyiwa chunguzi wa kimatibabu baada ya kuwasili katika kituo cha treni cha Munich, Septemba 7, 2015.
Wakimbizi wanafanyiwa chunguzi wa kimatibabu baada ya kuwasili katika kituo cha treni cha Munich, Septemba 7, 2015. REUTERS/Michaela Rehle

Wakimbizi wameendelea kuingi nchini Ujeremani kwa wingi wakipitia katika eneo la Eldorado. Jumamosi wiki hii, wakimbizi 13,000 ndio wamekua wakisubiriwa katika kituo cha treni cha Munich.

Matangazo ya kibiashara

Katika mji wa Munich, wakimbizi wanapowasili wamekua wakilindiwa usalama na kundi la watu wa kujitolea.

“ Kwa sasa mji wa miji ya Munich na Bavaria pekee haiwezi kukabiliana na changamoto hii kubwa ": viongozi wa mji wa kusini wa Ujerumani siku ya Jumamosi walitoakwa wito wa kusaidia kukabiliana na ongezeko linaloendelea la maelfu ya wakimbizi, ambapo kunakabiliwa ukosefu wa vitanda vya kutosha na maeneo ya huduma au sehemu za mapokezi.

Idadi hii ambayo ni sawa kwa udogo wake na rekodi iliyoorodheshwa Jumapili iliyopita kwa kipindi cha muda wa masaa 24. Mbali na kuwa hali ya kipekee, kama ilivyobainisha Berlin, ongezeko la wakimbizi mwishoni mwa wiki iliyopita ilikuwa mwanzo tu wa hali hii ambayo inaweza kuchukua muda mrefu.

Ni katika kituo cha Kati, karibu na kituo cha zamani wasafiri, ambapo imetengwa sehemu ya mapokezi kwa wakimbizi wanaoingia Ujerumani. Wakimbizi wanaopokelewa baada ya kushuka treni wanapewa chakula na vinywaji, kabla ya kufanyiwa uchunguzi wa afya na kisha kuwa kusafirishwa kwa basi, katika makaazi ya dharura.

Kwa sasa, hali ni shwari, lakini kama wanavyoasema watu wanaofanya kazi katika eneo hilo na ambao wako hapo kwa kusubiri wakimbizi, hali bado ni nzito. Hadi saa 10 alaasiri, wakimbizi 7219 walipita kwenye kituo cha treni cha Munich, na serikali ya Bavaria imekua ikikadiria kuwa hadi usiku wa manane, wengine angalau 3,000 wanaweza kufuata.