UGIRIKI-UCHAGUZI-SIASA

Ugiriki: chama cha Syriza chashinda uchaguzi wa wabunge

Baada ya kuhesabu nusu ya kura, chama cha mrengo wa kushoto chenye msimamo mkali kimeshinda kwa pointi 7.5 dhidi ya chama cha mrengo wa kulia ambacho kimechukua nafasi ya pili.

Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu anayemaliza muda wake, Alexis Tsipras, ametangaza kuundwa kwa serikali ya umoja na Anel, chama cha mrengo wa kulia.

Katika 53.61% ya kura zilizohesabiwa, chama cha Syriza kimepata 35.54% ya kura na viti 145 kwa jumla ya viti 300 katika bunge, dhidi ya chama cha mrengo wa kulia cha New Democracy, ambacho kimekua kimepta 28.11% na viti 75.

Kutokana na neema ya mgogoro wa wahamiaji, cham cha Golden Dawn kimechukua nafasi ya tatu nchini Ugiriki kwa kupata (7.09%ya kura na wabunge 19) mbele ya PASOK (wasoshalisti) ambacho kimepata (6.42% ya kura na wabunge 17), chama cha Kikomunisti cha KKE kimepata (5.48% ya kura na wabunge 15, chama cha mrengo wa kati cha Potami (3.93% ya kura na wabunge 10), chama cha Independent Greeks (3.68% na wabunge kumi) na cham cha Union of Centrists (3.43% na wabunge 10 ).

Panos Kammenos, kiongozi wa chama cha Independent Greeks, ambaye alishiriki katika serikali ya zamani ya Alexis Tsipras kati ya Januari na Agosti, ametangaza utayari wake wa kuungana na chama cha Syriza, ili kufanya muungano ambao utakua na wabunge wengi, sawa na viti 155 kwa jumla.

Kwa upande wake kundi la wabunge waliojitenga na cha cha Syriza kufuatia msimamo wao wa kupinga mpango mpya wa msaada kwa Ugiriki mwei Agosti mwaka huu, inaonekana kuwa kundi hilo halikupata mbunge hata mmoja, kwani kundi hili limepata chini ya 3% ya kura, kigezo kinacho hitajika ili kupata viti bungeni.