Pata taarifa kuu
UGIRIKI-SIASA-UHAMIAJI-UCHUMI

Ugiriki: Tsipras atawazwa kuwa Waziri Mkuu

Waziri Mkuu Alexis Tsipras (kushoto) wa chama cha mrengo wa kushoto  chenye msimamo mkali cha Syriza katika majadiliano na Rais wa Ugiriki, Prokopis Pavlopoulos, Septemba 21, 2015 katika mji wa Athens.
Waziri Mkuu Alexis Tsipras (kushoto) wa chama cha mrengo wa kushoto chenye msimamo mkali cha Syriza katika majadiliano na Rais wa Ugiriki, Prokopis Pavlopoulos, Septemba 21, 2015 katika mji wa Athens. Hélène COLLIOPOULOU | AFP
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Baada ya ushindi wake mkubwa katika baraza la wawakilishi, Alexis Tsipras Jumatatu wiki hii ameanza muhula wake wa pili kama Waziri mkuu wa Ugiriki baada ya kutawazwa.

Matangazo ya kibiashara

Alexis Tsipras anajianda kuongoza nchi ya Ugiriki akiwa pamoja na chama cha mrengo wa kulia katika serikali ya umoja, ambayo itakabiliwa na changamoto mbili ikiwa ni pamoja na sovereignist serikali ya umoja ambayo itakuwa mara moja kwa pande mbili: mageuzi magumu yanayosubiriwa na wakopeshaji wa Ugiriki na mgogoro wa uhamiaji.

Miezi minane baada ya uchaguzi wake wa kwanza mwezi Januari, Bw Tsipras ametawazwa kwa mara nyingine tena Jumatatu hii alaasiri kuwa Waziri mkuu akiapa kwa " heshima yake na dhamiri ", na wala sio " Injili " kama watangulizi wake wote.

Tsipras ameshinda uchaguzi wa Bunge wa Jumapili pili hii iliyopita katika kipindi cha miezi nane kwa 35.46% ya kura dhidi ya 28.10% ya chama cha mrengo wa kulia cha New Democracy.

Waziri Mkuu amesema anasubiri kuunda serikali yake Jumatano asubuhi ili asiwezi kukosa kikao cha Baraza la Ulayakiliyoitishwa siku hiyo mjini Brussels kuhusu mgogoro wa uhamiaji, akizungumzia kuwa faili hii ni kama moja ya vipaumbele vyake katika majadiliano yake na Rais wa Ugiriki, Prokopis Pavlopoulos pamoja na Waziri mkuu wa wa mpito Vasiliki Thanou.

" Hatimaye inawezekana kwamba Ulaya izingatiye wa wajibu wake mkubwa katika tatizo la Ulaya, ambalo haliwezi kutukabili pekee yetu, nchi za ukanda huu ", amesemaTsipras, ambapo nchi yake imekuwa lango kuu la kuingia barani Ulaya, huku akitoa wito kwa mshikamano zaidi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.