Pata taarifa kuu
UTURUKI-MASHAMBULIZI-USALAMA

Uturuki: watu 86 wauawa katika mashambulio mawili

Watu wakisaidia kuondoa miili ya watu waliouawa katika eneo la mashambulizi mawili yaliogharimu maisha ya watu 86  katika mji wa Ankara, Uturuki, Oktoba 10, 2015.
Watu wakisaidia kuondoa miili ya watu waliouawa katika eneo la mashambulizi mawili yaliogharimu maisha ya watu 86 katika mji wa Ankara, Uturuki, Oktoba 10, 2015. AFP/AFP
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Mashambulizi mawili yaliyolenga maandamano ya amani Jumamosi mjini Ankara, nchini Uturuki, na kusababisha vifo vya watu 86, yalitekelezwa na watu wawili waliojitoa mhanga, Waziri mkuu wa Uturuki, Ahmet Davutoglu, ametangaza.

Matangazo ya kibiashara

" Kuna ushahidi wa kutosha kwamba shambulio hilo limetekemezwa na watu wawili waliojitoa mhanga ", Waziri mkuu wa Uturuki Davutoglu amenbaini katika mkutano na waandishi wa habari.

Waziri mkuu wa Uturuki ametangaza ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa.

" Mashambulizi haya hayakulenga kundi la watu waliokuja kushiriki katika mkutano wa hadhara au jamii ya kisiasa, yamewalenga watu wetu wote , wakati ambapo tunaelekea katika uchaguzi (...) mashambulizi haya moja kwa moja yameilenga demokrasia yetu, haki zetu za msingi na uhuru wetu ", ameongezaAhmet Davutoglu,

Jumamosi hii asubuhi, milipuko miwili imepiga karibu na kituo kikuu cha magari jijini Ankara, ambapo maelfu ya wanaharakati kutoka nchini kote Uturuki walikua wameitikia wito wa vyama vingi vya wafanyakaz , mashirika yasiyo ya kiserikali na vyama vya mrengo wa kushoto vinavyounga mkono msimamo wa Wakurdi walioandamana kwa kukemea kuanza kwa mgogoro wa Kikurdi.

" Tunakabiliwa na moja ya vitendo vya kigaidi hatari katika historia ya Jamhuri yetu ", ameendelea Davutoglu, huku akikemea watu waliohusika na mashambulizi hayo ambao amewaita " maadui wa binadamu ".

Alipoulizwa kuhusu uzembe wa vikosi vya usalama, Davutoglu ameahidi kwamba hatua zote zimechukuliwa, akitangaza kwamba polisi iliwakamatwa hivi karibuni watu wawili waliotaka kujitoa mhangakatika mji ya Istanbul na Ankara.

Kiongozi huyo wa serikali amesema kuwa hakuna madai yoyote ambayo yameshamfikia kwa sasa. Lakini ametaja makundi matatuambayo yana uwezo wa kufanya mashambulizi hayo: waasi wa PKK, kundi la Islamic State (IS) na chama cha DHKP-C cha mrengo wa kushoto.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.