Pata taarifa kuu
UFARANSA-UGIRIKI-USHIRIKIANO

Hollande kulihutubia Bunge katika siku ya pili ya ziara yake Ugiriki

Alexis Tsipras na François Hollande Oktoba 22, 2015 jijini Athens.
Alexis Tsipras na François Hollande Oktoba 22, 2015 jijini Athens. FP/AF
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Rais wa Ufaransa François Hollande atakaribisha leo Ijumaa mbele ya Bunge la Ugiriki uamzi wa " kubaki katika Umoja wa Ulaya " wa Waziri Mkuu Kigiriki Alexis Tsipras, katika siku ya pili ya ziara yake nchini Ugiriki.

Matangazo ya kibiashara

Ziara hii ya Rais Hollande nchini Ugiriki inajikita kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, sayansi na utamaduni kati ya Paris na Athens.

Hotuba ya Rais Hollande, rais wa tatu wa Ufaransa kujieleza mbele ya Vouli, (Bunge la Ugiriki) baada ya jenerali de Gaulle mwaka 1963 na Nicolas Sarkozy mwaka 2008 inasubiriwa saa 16:00 saa za Ugiriki (sawa na saa 3:00 saa za kimataifa). Wakati fulani Ugiriki ilikabiliwa na hali ya sintofahamu katika uchumi wake, ambapo baadhi ya raia wa nchi hiyo walifikia kuchukua uamzi wa kujiondoa katika Umoja wa Ulaya, na hivyo kutishia mshikamano wa Ulaya. Kwa mujibu wa wasaidizi wake, Rais wa Ufaransa, atakaribisha ujumbe aliyoutoa alexis Tsipras katika jengo hilo, akiwasihi wabunge kuepuka kuiondoa nchi yake katika kundi la nchi za Umoja wa Ulaya.

Alhamisi alipowasili katika mji wa Athens, Rais Hollande alikumbusha " maamuzi ya ujasiri " yaliyochukuliwa na kiongozi wa serikali ya Ugiriki, kiongozi wa kwanza barani Ulaya kutoka mrengo wa kushoto wenye msimamo mkali, ambaye alikubali mwezi Julai mpango mpya wa msaada.

Rais wa Ufaransa ameongozona na mawaziri wanne. Mazungumzo yatafanyika kati ya ujumbe kutoka serikali hizo mbili.Mkutano huu utakuwa ni fursa ya kujadili biashara, lakini pia Ugiriki inasubiri msaada wa Ufaransa kuhusu suala la madeni.

" Tulifanya, Ufaransa na Ugiriki, kilicho kuwa chini ya uwezo wetu (...) ili Ugiriki uendelee kubaki katika Umoja wa Ulaya na kwamba Ulaya ishikamane na Ugiriki. Na hata leo, ujumbe huo ndio ntaendelea kutoa ", pia amehakikisha rais wa Ufaransa, huku akiomba " kuanza kwa mazungumzo " kupitia " kuahirishwa kwa maslahi "ya madeni ya Athens, ambayo ni karibu 200% ya Pato la Taifa.

Rais Hollande pia ameunga mkono ombi la Viongozi wa Ugiriki na Umoja wa Ulaya kwa kuongeza Euro milioni 330 mwaka 2016 kwa kukabiliana na ongezeko la wahamiaji, ambao walikuwa zaidi ya 500,000 kuwasili nchini Ugiriki tangu Januari mwaka 2015.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.