Pata taarifa kuu
CHINA-NORWAY-IS-MAUAJI

IS yatangaza kuwaua mateka wa China na Norway

Mpiganaji wa kundi la Islamic State akishikilia bendera nyeusi ya Islamic State, karibu na mpaka wa Iraq na Syria.
Mpiganaji wa kundi la Islamic State akishikilia bendera nyeusi ya Islamic State, karibu na mpaka wa Iraq na Syria. ALBARAKA NEWS / AFP
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Kundi la Islamic State limetangaza Jumatano wiki hii kuwa limewaua mateka wawili, miezi miwili baada ya kudai fidia kwa ajili ya kuachiliwa kwao.

Matangazo ya kibiashara

Kundi hi la IS limetangaza kkuwa limewamalizi maisha mateka wawili, mmoja kutoka China na mwengine Norway. Tangazo hilo limechapishwa katika toleo la hivi karibuni la gazeti la propaganda la kundi la Islamic State, Dabiq, lililorushwa kwenye mtandao Jumatano wiki hii.

Tarehe 10 Septemba mwaka huu, kundi la IS lilitangaza kwa mara ya kwanza kushikilia mateka hao wawili bila kutaja lini na wapi waliotekwa nyara. Katika gazeti lake, kundi hili kijihadi lilitangaza likimtaka mtu yeyote "ambaye anataka kulipa fidia kwa ajili ya kuachiliwa na kusafirishwa kwa watu hawa wawili ", ambao picha zao zilirushwa kwenye mitandao. Norway ilithibitisha utekaji nyara wa mmoja wa raia wake, Ole-Johan Grimsgaard-Ofstad, muda mfupi baada ya kuwasili nchini Syria mwishoni mwa mwezi Januari mwaka 2015, lakini ilikataa kulipa fidia. Haikujulikana kwa sababu za uwepo wa raia huyo wa Norway nchini Syria. China pia ilikiri kwamba moja wa raia wake alikua mikononi mwa kundi la Islamic State (IS).

Jumatano hii, katika toleo lake la 12, gazeti la Dabiq limeweka picha za miili ya mateka hao wawili, huku wakijaa damu usoni, na kufunikwa na utepe mkubwa wa rangi njano kichwani, ambapo kuliandika "kunyongwa baada ya kutelekezwa na mataifa na mashirika yasio waaminifu".

IS, ambayo hutumia picha ya mauaji yake kama kifaa cha propaganda, katika siku za nyuma ilikua ikirusha hewani video inayoonyesha mateka wengi wanavyouawa, hususan mateka kutoka nchi za Magharibi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.