UBELGIJI-USALAMA-UGAIDI

Hali ya hatari bado yashuhudiwa Brussels

Waziri mkuu Charles Michel Novemba 22, 2015 jijini Brussels.
Waziri mkuu Charles Michel Novemba 22, 2015 jijini Brussels. JOHN THYS/AFP

Mji wa Brussels bado ni unakabiliwa na hali ya hatari, huku viongozi wakitoa tahadhari nyingine. Jumatatu Novemva 23, shughuli zitasitishwa katika maeneo mbalimbali.

Matangazo ya kibiashara

Jeshi limeagizwa kuuzingira mji huo kufuatia vitisho vya mashambulizi sawa na yale ya Paris.

Hali ya sintofahamu imeendelea kushuhudiwa katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels na katika miji mji mikuu barani Ulaya ambapo wahusika wa mashambulizi yaliotokea usiku wa Novemba 13 jini Paris wanaendelea kusakwa.

Baada ya kushauriana na vyombo vya usalama, uamuzi wa kuendelea na hali ya tahadhari ya ugaidi katika kiwango cha juu umechukuliwa katika mkoa wa Brussels (wenye wakazi milioni 1.2) na "kupunguza matukio makubwa (kama sherehe), kuendelea kufungwa kwa vituo vya treni za mwendo kasi ", Waziri mkuu wa Ubelgiji Charles Michel , ametangaza Jumapili hii jioni.

"Shule zitafungwa Jumatatu hii mjini Brussels", Charles Michel ameongeza. Jambo ambalo halijawahi kushuhudiwa katika nchi hiyo kifalme. Tathmini mpya ya kiwango cha tahadhari itafanyika Jumatatu hii mchana.