UHISPANIA-MAANDAMANO-USALAMA-SHERIA

Maandamano yafanyika Madrid kwa kutambua uhalifu wa Franco

Maandamano ya kutaka kutambuliwa kwa uhalifu uliotekelezwa na Francisco Franco, kiongozi wa zamani wa Uhispania yamefayika Jumapili Novemba 22, 2015.
Maandamano ya kutaka kutambuliwa kwa uhalifu uliotekelezwa na Francisco Franco, kiongozi wa zamani wa Uhispania yamefayika Jumapili Novemba 22, 2015. REUTERS/Juan Medina

Maelfu ya watu wameandamana katika mitaa ya mji wa Madrid Jumapili Novemba 22, na kudai kutambua uhalifu wa udikteta wa Francisco Franco, ambaye alifariki miaka 40 iliyopita, aliyepewa msamaha uliopitshwa mwaka 1977.

Matangazo ya kibiashara

Mbele ya msafara huo, kulionekana bango lililoandikwabendera alitangaza kauli mbiu ya "ukatili uliotekelezwa na Franco, unatosha!".

Waandamanaji wamekua wakidai kufutwa kwa sheria ya msamaha ya mwaka 1977, miaka miwili baada ya kifo cha dikteta huyo, sheria ambayo inazuia hatua za kisheria dhidi ya wahusika wa ukiukaji wa haki za binadamu wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Uhispania na chini ya udikteta wa Francisco Franco. Katika maandamano hayo kumeonekana bendera za chama cha Republican. Franco aliongoza vita vy kijeshi dhidi ya Uhispania mwaka 1936 na kuendesha machafuko yaliosababisha vifo vya watu wengi baada ya ushindi wake mwaka 1939, na baada ye kuongoza nchi hiyo peke yake hadi kifo chake Novemba 20, 1975.

Baadhi ya vyama vya kisiasa vimepinga kukumbushia matukio mabaya yaliotokea nchini Uhispani miaka iliyopita.

Miongoni mwa maelfu ya walioshiriki maandamano hayo, wazee wengi walibebelea bango llililokua limeandikwa jina la mtu mzima aliyeuawa wakati wa utawala wa kidikteta wa Franco. Waandamanaji wameomba sheria ya msamaha ifutwe na kutekeleza sheria ya kumbukumbu ya kihistoria iliyopitishwa mwaka 2007 na serikali ya Kisochalisti, lakini haifanyi kazi tangu kuingia madarakani kwa Mariano Rajoy kutoka chama cha Conservative mwaka 2011.

Sheria ya kumbukumbu ya kihistoria inabaini kufutwa kwa alama zilizokua zikitumiwa katika utawala wa kidikteta wa Franco ambazo zipo na kusaidia familia ambazo zinataka kupata miili ya mababu zao iliozikwa katika makaburi ya pamoja. Chama cha Waziri mkuu wa sasa Mariano Rajoy, mrithi wa vyama vya mrengo wa kulia vilivyoundwa baada ya udikteta, anakataa "kukumbushia matukio mabaya yaliotokea katika miaka iliyopita" na kusema kuwa kunahitajika kutumia sheria ya msamaha au kutumia sheria ya kumbukumbu ya kihistoria.

Maadhimisho ya kifo cha Franco hakusherehekewa na vyama vikuu vya kisiasa, bali vyama vidogo tu.