Pata taarifa kuu
UFARANSA-MAREKANI-UGAIDI-MAUAJI-USALAMA

François Hollande ziarani Marekani

François Hollande njiani kuelekea Marekani kwa mazungumzo na Barack Obama.
François Hollande njiani kuelekea Marekani kwa mazungumzo na Barack Obama. AFP PHOTO / POOL / STEPHANE DE SAKUTIN
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Rais wa Ufaransa François Hollande anaelekea nchini Marekani leo Jumanne kukutana na mwenyeji wake rais Barrack Obama kujadiliana mbinu za kupambana na ugaidi duniani baada ya shambulizi la jijini Paris.

Matangazo ya kibiashara

Ziara hii inakuja baada ya Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron kuzuru Paris Jumatatu wiki hii na kufanya mazungumzo na Rais Hollande na kuahidi kuwa nchi yake itashirikiana na Ufaransa kupambana na ugaidi.

Rais Hollande pia atazuru Urusi kwenda kukutana na rais Vladimir Putin na baadaye Ujerumani kuzungumza na Kansela Angela Merkel.

Lengo ni kutafuta muungano wa kupambana na Islamic State magaidi wanaoendelea kutishia usalama wa dunia.

Wakati huo huo Marekani imetoa tangazo kwa raia wake kuwa makini wanaposafiri katika nchi mbalimbali duniani kutokana na ongezeko la mashambulizi ya kigaidi.

Tahadhari hii itasalia hadi tarehe 24 mwezi Februari mwaka ujao.

Hatua hii inakuja baada ya mashambulizi ya Islamic State nchini Ufaransa wiki mbili zilizopita, mashambulizi ya mara kwa mara ya Boko Haram, Al Shabab na yale ya Al Qaeda Kaskazini mwa Afrika.

Marekani imesisitiza kuwa raia wake wanaozuru Ubelgiji kuwa makini kutokana na wasiwasi wa kutokea kwa mashambulizi katika jiji la Brussels.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.