Pata taarifa kuu
UFARANSA-UJERUMANI-USHIRIKIANO

Merkel aahidi hatua za kijeshi dhidi ya Daech

Angela Merkel (ushoto) zirani Paris akiambatana na Hollande (kulia), Novemba 25, 2015.
Angela Merkel (ushoto) zirani Paris akiambatana na Hollande (kulia), Novemba 25, 2015. AFP/Etienne Laurent
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Baada ya kutembelea katika eneo la Jamhuri mjini Paris katika kumbukumbu ya waathirika wa Novemba 13, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameahidi "hatua za haraka" kwa ugaidi.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufaransa François Hollande na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel walijielekeza pamoja muda mfupi baada ya saa 12 jioni saa za Paris katika eneo la Jamhuri mjini Paris, ambapo kila mmoja aliweka ua kwa heshima ya waathirika 130 wa mashambulizi ya Novemba 13. Kisha Viongozi hao wawili walifanya mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya Elysée.

Baada ya Washington, ambapo Rais wa Ufaransa alijaribu kupata msaada zaidi kwa mapambano dhidi ya kundi la Islamic State, hatimaye kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema yuko tayari kushirikiana na Ufaransa kwa kulitokomeza kundi hilo.

"Tunapaswa kushughulikia sababu", "tunapaswa kupambana dhidi ya Daech", amesisitiza François Hollande, ni kwa mantiki hiyo alikubaliana na rais wa Marekani Barack Obama kuzidisha mashambulizi".

Merkel ametangaza kwamba Ujerumani iko tayari kupeleka askari zaidi nchini Mali ili kuiwezesha Ufaransa kuweka majeshi yake mahali pengine. Hollande amesisitiza: "Napenda Ujerumani ijihusishe na suala hili zaidi", na mawaziri wa ulinzi wa Umoja wa Ulaya pia kufanya hivyo. "Tutakuwa pamoja na Ufaransa", amesema Merkel, ambaye aliahidi kuchukua hatua "haraka". "Tutachukua hatua za haraka, kwa sababu tunataka kupigana kwa pamoja dhidi ya ugaidi, ni dhamira yetu, ni wajibu wetu, ni lazima tuchukue hatua kwa kujituma. Daech, hatuwezi kuishinda kwa maneno, itachukua njia ya kijeshi",amesema Kansela.

Pia kulizungumziwa suala la wakimbizi. François Hollande amesifu juhudi za Ujerumani katika sula la mapokezi ya watu waliokimbia vita na kundi la Islamic State, huku akikumbusha nia yake ya kuepuka kufananisha wakimnbizi na ugaidi na ametoa wito wa kuwa makini katika udhibiti wa mipaka ya nje ya Ulaya.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.