FIFA-SOKA-UFISADI

Wimbi jipya la kukamatwa kwa viongozi wa FIFA nchini Uswisi

Wimbi jipya la kukamatwa kwa maafisa kadhaa, wa sasa na wa zamani, wa Shirikisho la kimataifa la Soka (FIFA) limefanyika Alhamisi hii asubuhi nchini Uswisi, gazeti la New York Times limearifu katika mtandao wake.

Nembo ya Shirikisho la kimataifa la Soka (FIFA) mbele ya shirikisho hilo mjini Zuric Oktoba 8, 2015.
Nembo ya Shirikisho la kimataifa la Soka (FIFA) mbele ya shirikisho hilo mjini Zuric Oktoba 8, 2015. AFP/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Operesheni hii imefanyika kwa ombi la vyombo vya sheria vya Marekani na inafanyika miezi saba baada ya wimbi la kwanza la kukamatwa kwa maafisa wengine kwa kosa la udanganyifu, rushwa na kujitajirisha kinyume cha sheria kwa watu kumi na nane, ikiwa ni pamoja na viongozi wa FIFA.

Operesheni imeanza saa 12:00 asubuhi (sawa na saa 500 asubuhi saa za kimataifa) na imelenga hoteli Baur, kulikoshuhudiwa wimbi la kwanza la kukamatwa kwa maafisa wa FIFA tarehe 27 Mei, 2015.

Sepp Blatter, rais wa FIFA aliyejiuzulu na kusimamishwa, si miongoni mwa wale waliokamatwa katika mji wa Zurich, gazeti la New York Times limebaini.

Gazeti hili la kila siku la Marekani limearifu kuwa waliolengwa na operesheni hiyo kwa kiasi kikubwa walikua wawakilishi wa mashirikisho ya soka ya Amerika ya Kusini na Amerika ya Kati.

New York Times pia imearifu, ikinukuu vyanzo ambavyo haikuvitaja kwamba mahakama ya Marekani ingelianzisha utaratibu wa mashitaka Alhamisi hii asubuhi.

Kama mwezi Mei, operesheni hii inatokea wakati ambapo Fifa Shirikisho la kimataifa la Soka (FIFA) linakutana Kamati yake tendaji kwa muda wa siku mbili, Desemba 2 na 3 katika mji wa Zurich.

Wakati wa mkutano wa Kamati tendaji, FIFA inatazamiwa kushughulikia mageuzi muhimu kwa ajili ya hatma yake kufuatia kashfa iliyozuka mwezi Mei kwa ombi la vyombo vya sheria vya Marekani.

Wachunguzi wa Marekani walibaini kwamba viongozi wa soka duniani walipokea rushwa katika katika zoezi la hatua za mwisho za kukabidhi Kombe la Dunia na matangazo ya biashara kwa runinga mbalimbali duniani.