USWISI-UGAIDI-USALAMA

Tishio la kigaidi: Geneva katika hali ya hatari

Kiwango cha tahadhari kimewekwa alhamisi wiki hii mjini Geneva. Viongozi wa Uswisi wamepata taarifa ya harakati za hivi karibuni katika ardhi ya nchi hiyo za watu sita wanaoshukiwa kuwa na msimamo mkali au kuwa na uhusiano na kundi la Islamic State.

Askari polisi katika mlango wa uwanja wa ndege wa Geneva, Desemba 10, 2015.
Askari polisi katika mlango wa uwanja wa ndege wa Geneva, Desemba 10, 2015. REUTERS/Pierre Albouy
Matangazo ya kibiashara

Hofu ya kutokea kwa mashambulizi, pengine dhidi ya Umoja wa Mataifa imetanda katika mji huo.

Vikosi vya usalama vimeimarisha ulinzi katika mji wa Geneva na huku doria ikipigwa katika maeneo mbalimbali, ukaguzi mkali umeendelea kushuhudiwa kwenye mipaka ya nchi hiyo. Askari polisi wameonekana kwa wingi katika mji wa Geneva Alhamisi wiki hii, ikiwa ni pamoja na kwenye maeneo muhimu kama vile pembezoni mwa jengo la Bunge.

Wafanyakazi wameondolewa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi kwa ajili ya ukaguzi wa majengo.

Itafahamika kwamba mkutano kuhusu Syria utafanyika Ijumaa hii kati ya Urusi, Marekani na upinzani wa Syria. Ni vigumu kutofanya uhusiano wa watu hawa sita wanaotafutwa

Mshirika wa karibu wa Salah Abdeslam ni miongoni mwa watuhumiwa?

Wanne kati watu hao sita wanasadikiwa kuunga mkono kundi la Islamic State.

Wengine wawili wanasakwa na Ufaransa, wakituhumiwa kuwa na msimamo mkali. Watu hao walionekana jijini Geneva Jumanne iliyopita wakiwa katika gari ndogo aina ya Pickup yenye usajili wa Ubelgiji, kabla ya kutimka.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa, mmoja wa watu wawili anaweza kuwa mshirika wa karibu wa Salah Abdeslam, aliyelishiriki katika mashambulizi ya Novemba 13 mjini Paris na bado hawajakamatwa.

Viongozi wa Uswisi wamewataka raia kuwa makini na kuzidisha ushirikiano wao na vikosi vya usalama.