VYOMBO VYA HABARI

Waandishi wa habari 67 wauawa mwaka 2015

Waandishi wa habari sitini na saba waliuawa duniani kote mwaka 2015 kwa sababu ya taaluma yao pamoja na "raia 27 wanaojihusisha na taaluma ya uandishi wa habari" (wanablogu) na wasaidizi 7 wa vyombo vya habari, kwa mujibu wa ripoti ya mwaka ya Waandishi Wasio na Mipaka (RSF) iliyotolewa Jumanne hii.

Kadi ya waandishi wa habari ikiwa na maandishi "mimi ni Charlie" Januari 8, 2015 katika Brussels.
Kadi ya waandishi wa habari ikiwa na maandishi "mimi ni Charlie" Januari 8, 2015 katika Brussels. AFP/BELGA/AFP/
Matangazo ya kibiashara

Waandishi wa habari 66 waliuawa mwaka 2014, kwa mujibu wa RSF. Iraq na Syria ni miongoni mwa nchi ambapo waandishi wa habari wengi waliuawa mwaka 2015, ikifuatiwa na Ufaransa, ambayo inachukua nafasi ya 3 kutokana na mashambulizi ya mwezi Januari dhidi ya gazeti la kila wiki la Charlie Hebdo.

Kwa ujumla waandishi wa habari 110 waliuawa mwaka 2015 katika mazingira mbalimbali. Tangu mwaka 2005 waandishi wa habari 787 waliuawa duniani kote.

Christophe Deloire, Katibu mkuu wa RSFanasema kwamba "ni muhimu kwa kuweka utaratibu madhubuti kwa ajili ya utekelezaji wa sheria za kimataifa juu ya ulinzi wa waandishi wa habari." "Leo hii, makundi mbalimbali yanajihusisha na mauaji dhidi ya waandishi wa habari, wakati ambapo nchi nyingi haziheshimu majukumu yao", ameongeza Christophe Deloire.

"Waandishi wa habari 110 waliuawa mwaka huu wanapaswa kuwa wanahabari wa mwisho kuuawa na taasi za kimataifa zinahitajika kuchukua hatu za haraka bila kuchelewa. "Mwakilishi maalum kwa ajili ya ulinzi wa waandishi wa habari chini ya usimamizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anapaswa kuteuliwa bila kuchelewa", amebaini Katibu mkuu wa shirika la Waandishi wa habari Wasio na Mipaka.