Pata taarifa kuu
UTURUKI-ULAYA-MASHAMBULIZI

Vitisho: watu 2 wakamatwa Uturuki, Ulaya katika hali tahadhari

Askari wakipiga doria usiku katika ufunguzi wa sikukuu ya Krismasi katika mji Brussels, Novemba 27, 2015.
Askari wakipiga doria usiku katika ufunguzi wa sikukuu ya Krismasi katika mji Brussels, Novemba 27, 2015. AFP/AFP/
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Vitisho vya ugaidi vinavyoendelea kushuhudiwa katika siku hizi za sikukuu za mwisho wa mwaka vimepelekea vikosi vya usalama kuwa katika hali ya tahadhari katika nchi kadhaa, ikiwa ni pamoja na Uturuki, ambapo mashambulizi ya kujitoa mhanga yalitibuliwa jijini Ankara.

Matangazo ya kibiashara

Brussels imeamua kufuta sherehe hizo za sikukuu. Hatua za usalama pia zimeimarishwa katika nchi nyingine, kama vile Austria na Urusi baada ya mashambulizi ya Novemba 13 mjini Paris, mji ambao utakuwa chini ya ulinzi mkali wa polisi Alhamisi hii usiku.

Jumatano hii, polisi ya Uturuki imewatia mbaroni wanamgambo wawili wanaoshukiwa kuwa wa kundi la Islamic State (IS) ambao wanatuhumiwa kupanga mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga katika mji wa Ankara wakati wa sikukuu za mwisho wa mwaka.

"Katika mfumo wa uchunguzi ulioanzishwa na Ofisi ya mashitaka ya Ankara na kazi iliyofanywa na polisi ya Ankara, watu wawili, ambao ni wanamgambo wa kundi la Islamic State wamekamatwa wakati wa operesheni yenye mafanikio kabla ya kutekeleza mashambulizi",manispaa ya mji mkuu wa Uturuki imesema katika tangazo liliorushwa hewani.

"Vilipuzi kadhaa viliokuwa tayari kwa matumizi na mkoba uliojazwa mabomu na mkanda wa kujilipua vimekamatwa" na polisi wakati wa operesheni, tangazo hilo limebaini.

Watuhumiwa hao wawili wamekua wakijianda kufanya mashambulizi ya kujitoa mhanga Alhamisi hii usiku katika maeneo mawili (mbele ya kituo cha biashara na katika mtaa ulio karibu na eneo hilo) cha eneo la kati la Kizilay, eneo la jadi la sikukuu za Mwaka Mpya, kwa mujibu wa vituo vya televisheni vikinukuu Ofisi ya Mwendesha mashitaka mkuu wa Ankara, mji wa pili kwa ukubwa nchini Uturuki, wenye wakazi milioni 5.2 baada ya Istanbul.

Maelfu ya watu hukusanyika katika eneo hilo la kijadi kusherehekea kuwasili kwa mwaka mpya.

Uturuki imewekwa katika hali ya tahadhari tangu mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga yaliosababisha vifo vya watu 103 na zaidi ya 500 kujeruhiwa mbele ya kituo kikuu cha treni mjini Ankara Oktoba 10.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.