UTURUKI-PKK-MAUAJI

Uturuki: mwanamke auawa kwa kombora kusini mashariki

Familia, ndugu na marafiki wa mwanamke aliyeuawa na shambulio la kombora juu kwenye nyumba yake, katika mji wa Diyarbakir, kusini mashariki mwa Uturuki, 3 Januari 2016.
Familia, ndugu na marafiki wa mwanamke aliyeuawa na shambulio la kombora juu kwenye nyumba yake, katika mji wa Diyarbakir, kusini mashariki mwa Uturuki, 3 Januari 2016. AFP/AFP

Mama wa watoto watatu ameuawa Jumapili hii kwa kombora katika mji mkubwa unaokaliwa na Wakurdi wengi wa Diyarbakir, kusini mwa Uturuki, eneo ambalo linakabiliwa na mapigano kati ya Ankara na waasi wa PKK, shirika la habari Dogan limearifu.

Matangazo ya kibiashara

Melek Alpaydin, miaka 38, alikuwa akipata chakula wakati kombora lilipoanguka katika nyumba yake, kwenye ghorofa ya pili ya jengo dogo, na kumua na kumjeruhi mtu mwingine.

Kwa mujibu wa shirika la habari Dogan, uchunguzi unaendelea ili kujua chanzo cha tukio hilo.

"Mji mkuu" wa Kusini unaokaliwa na Wakurdi wengi nchini Uturuki, Diyarbakir, ni eneo la mapigano mbalimbali tangu kuanza kwa mapigano kati ya waasi wa PKK na vikosi vya usalama vya Kituruki, katika majira ya joto mwaka uliyopita.

Amri ya kutotoka nje iliwekwa Desemba 2 katika kitongoji cha Sur, katikati mwa mji wa Diyarbakir, ambapo alikua akiishi mwanamke huyo.

Kwa mujibu wa chama kiachounga mkono Wakurdi (HDP), raia kumi na mbili wameuawa katika wilaya ya Sur tangu kuanza kwa operesheni ya vikosi vya serikali dhidi ya waasi wa Kikurdi wa PKK.