UTURUKI-VYOMBO VYA HABARI

Uturuki: mwandishi wa habari wa Iraq aachiwa huru

Askari polisi wa Uturuki akipiga doria katika mji wa Diyarbakir, kusini mashariki mwa Uturuki, Desemba 30, 2015.
Askari polisi wa Uturuki akipiga doria katika mji wa Diyarbakir, kusini mashariki mwa Uturuki, Desemba 30, 2015. AFP/AFP/

Mahakama nchini Uturuki imemuachia huru Jumanne hii mwaandishi wa habari wa Iraq, aliokua akiifanya kazi katika timu ya mtandao wa habari wa Vice News.

Matangazo ya kibiashara

Mohammed Ismael Rasool alikamatwa nchini Uturuki mwishoni mwa mwezi Agosti wakati alipokua akichunguza habari kuhusu mgogoro wa Wakurdi, chanzo cha mahakama kimeeleza.

Mohammed Ismael Rasool aliwekwa chini ya ulinzi na kufungwa Agosti 31 na mahakama ya mji wa Diyarbakir, mji mkubwa kusini mashariki mwa Uturuki wenye wakazi wengi kutoka jamii ya Wakurdi, pamoja na waandishi wa habari wawili kutoka Uingereza wa timu hiyo ya mtandao wa habari wa Vice News, Jake Hanrahan na Philip Pendlebury.

Wawili hawa waliachiwa huru Septemba 3.

Mohammed Ismael Rasool ameachiwa huru kwa masharti ya kutoondoka katika ardhi ya Uturuki hadi mwisho wa kesi yake, ambapo tarehe ya kesi hiyo kusikilizwa tena haijatolewa, chanzo cha mahakama kimeendelea.

"Timu ya mtandao wa habari wa Vice News ina Furaha ya kuthibitisha kwamba mwandishi wake Mohammed Rasool ameachiwa huru kwa dhamana baada ya kushikiliwa kwa muda wa siku 131 gerezani nchini Uturuki", kimejibu chombo hiki cha habari katika taarifa yake, ambapo makao yake makuu yapo nchini Marekani. "Rasool sasa ana furaha ya kuwa tena na famile yake, marafiki na wafanyakazi wenzake", chambo hicho kimeongeza.