UJERUMANI-WAKIMBIZI

Merkel ataka kupunguza wimbi la wakimbizi barani Ulaya

Berlin, Ofisi ya Mambo ya Jamii na Afya.
Berlin, Ofisi ya Mambo ya Jamii na Afya. REUTERS/Hannibal Hanschke

Merkel anataka kupunguza wimbi la wakimbizi katika Umoja wa Ulaya, huku akitaka mipaka ifunguliwe katika nchi wanachama wa Umoja huo.

Matangazo ya kibiashara

"Ni muhimu sana kwangu kufikira kwa pamoja kupunguza wimbi kubwa la wakimbizi na, wakati huo huo, kuhifadhi uhuru wa watu wa kutembea katika nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya", Kansela wa Ujerumani amesema mbele ya vyombo vya habari Jumatano hii katika mkutano wa chama cha CSU, kinachounga mkono chama chake cha CDU.

Uhuru wa kutembea, unavyoelezwa katika nchi za jumuiya ya Schengen ulikuwa ni "hatua kubwa ya maendeleo ya kiuchumi na ustawi."

Merkel ameongea hayo siku mbili baada ya Denmark na Sweden kuchukua uamzi wa udhibiti katika mipaka yao.

Zaidi ya watu milioni moja waliokimbia Mashariki ya Kati na Afrika waliwasili Ulaya mwaka 2015, Ujerumani ikiwa ndio nchi wanayolenga. Ujerumani, vinasema vyanzo vya serikali mjini Berlin na kutoka vyombo vya habari vya Ujerumani, imepokea takriban milioni 1.09 ya watu wanaotafuta hifadhi mwaka jana.

Serikali ya Ujrumani pia haijaona idadi ya wakimbizi waliowasili katika ardhi yake inapungua pamoja na jitihada za Umoja wa Ulaya kwa kukabiliana na ongezeko la wahamiaji, amesema Jumatano hii Naibu waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani, Ole Schroder.