FIFA-PLATINI-UCHAGUZI

Soka: Platini ajiondoa kwenye kinyan'ganyiro cha urais wa FIFA

Michel Platini, mwezi Agosti 2014, katika mji wa Monte Carlo.
Michel Platini, mwezi Agosti 2014, katika mji wa Monte Carlo. REUTERS/Eric Gaillard/Files

Michel Platini ameamua kujiondoa katika kinyan'ganyiro cha urais wa Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA), uchaguzi ambao umepangwa kufanyika Februari 26, amesema katika mahojiano na gazeti la Equipe (Timu).

Matangazo ya kibiashara

Mfaransa huyo, aliyesimamishwa kwa kipindi cha miaka 8 na FIFA, amebaini kwamba hana muda wa kufanya kampeni, hata kama angelirejeshewa hadhi yake na Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo.

"Sintogombea kama rais wa FIFA (Shirikisho la Kimataifa la Soka). Ninajiondoa  katika kinyan'ganyiro hicho". Michel Platini ameamua kuachia ngazi. Ametangaza katika mahojiano na gazeti la Equipe litakalochapishwa Januari 8, 2016.

Muda mfupi mno

"Siwezi, sina muda wala uwezo wa kwenda kuwaona wapiga kura, kukutana na watu wengine muhimu, wala muda wa wa kupambana na wengine", amesema mchezaji huyo wa zamani.

Kugombea kwa Michel Platini kwenye nafasi ya urais wa FIFA hakungepokelewa kama Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo haingelifuta uamzi huo kabla ya Januari 26. Muda ambao halikubaliki kwa mkuu wa zamani wa Shirikisho la Soka barani Ulaya (UEFA).

"Kwa kujiondoa kwangu, ninajipa muda wa wa kuandaa utetezi kuhusu kesi inayonikabili ikilinganishwa na kesi ambayo inazungumzia tu rushwa, kughushi, ambapo hakuna jambo jingine", Michel Platini amesema katika mahojiano na gazeti la Equipe.