UTURUKI-SHAMBULIO

Uturuki: shambulio la kujitoa mhanga Istanbul

Eneo kulikotokea shambulio la kujitoa mhanga limefungwa na vikosi vya usalama, Jumanne Januari 12 katika mji wa kale wa Sultanahmet, karibu na Msikiti wa Blu na eneo la St Sophia, Istanbul.
Eneo kulikotokea shambulio la kujitoa mhanga limefungwa na vikosi vya usalama, Jumanne Januari 12 katika mji wa kale wa Sultanahmet, karibu na Msikiti wa Blu na eneo la St Sophia, Istanbul. REUTERS/Kamal Aslan

Mlipuko mkubwa umetokea Jumanne hii Januari 12, 2016 katika kituo cha utalii cha Sultanahmet katika mji wa Istanbul, karibu na Msikiti wa Blu na makavazi ya St Sophia.

Matangazo ya kibiashara

Watu wasiopungua 10, wengi wao wakiwa Wajerumani wameuawa, na wengine 15 wamejeruhiwa. Waziri mkuu amesema kuwa mshambuliaji, ni raia wa Syria, ambaye alizaliwa mwaka 1988, na ni mwanamgambo wa kundi la Islamic State.

Shambulio lililotokea Jumanne hii asubuhi limeligusa eneo lenye ishara kubwa katikati mwa mji wa Istanbul, eneo ambalo ni la kitalii la Sultanahmet. Kwa mujibu wa mwandishi wetu katika mji wa Istanbul, Alexander Billet, mlipuko huo ulikua mkubwa kwani ulisikika hata katika miji mbalimbali jirani barani Asia.

Waathirika wengi ni Wajerumani

Vyombo vya habari vya Uturuki awali vilibaini kuwa watu kadhaa walijeruhiwa, wala hakuna aliyepoteza maisha, lakini mlipuko huo umesababisha vifo vya watu wasiopungua 10. Wengi wa watu waliopoteza maisha ni wageni. Mapema mchana, Waziri mkuu wa Uturuki, Ahmet Davutoglu, amewasiliana na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ili kumuarifu kuwa wengi mwa waliopoteza maisha ni raia wa Ujerumani. Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani imewashauri raia wake kuepuka maeneo ya kitalii ya Istanbul. Ubalozi wa Norway umesema kuwa mmoja wa raia wake ni pia miongoni mwa watu waliopoteza maisha.

Waziri mkuu Ahmet Davutoglu ameendesha mkutano kuhusu hali hiyo Jumanne hii asubuhi na waziri wa mambo ya ndani pamoja na mkuu wa Idara ya Ujasusi. Kwa mujibu wa Naibu Waziri mkuu wa Uturuki Numan Kurtulmus, mamlaka ya nchi hiyo imemtambuliwa muhusika wa shambulio hilo, mshambuliaji wa kujitoa mhanga anayeelezwa kuwa ni raia wa Syria, ambaye alizaliwa mwaka 1988. Katika hotuba fupi kwenye runinga ya taifa, Ahmet Davutoglu amesema kuwa ni mwanamgambo wa kundi la Islamic State. Mapema mchana, wakati wa hotuba yake kwa taifa, rais wa Uturuki mwenyewe amelaani "shambulio hilo la kujitoa mhanga".

Polisi inatoa ulinzi katika eneo kulikotokea mlipuko karibu na eneo takatifu la St Sophia na Msikiti wa Blu, Januari 12, 2016.
Polisi inatoa ulinzi katika eneo kulikotokea mlipuko karibu na eneo takatifu la St Sophia na Msikiti wa Blu, Januari 12, 2016. Reuters