UTURUKI-PKK-SHAMBULIO

Uturuki: watu 6 wauawa katika shambulio la waasi wa Kikurdi kusini mashariki

Askari polisi wa Uturuki katika mji wa Diyarbakir, Desemba 24, 2015.
Askari polisi wa Uturuki katika mji wa Diyarbakir, Desemba 24, 2015. AFP/AFP/

Watu sita wameuawa na wengine 39 wamejeruhiwa Alhamisi hii kusini mashariki mwa Uturuki katika shambulio la bomu lililotegwa ndani ya gari, shambulio ambalo linadaiwa kutekelezwa na waasi wa Kikurdi.

Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo linatokea siku mbili baada ya shambulio lililodaiwa kutekelezwa na kundi Islamic State (IS) na kuuawa watalii 10 kutoka Ujerumani mjini Istanbul.

Kulingana na taarifa ziliotolewa awali na kutolewa kwa mamlaka ya mkoa wa Diyarbakir, mlipuko huo uliotokea usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi ulilenga makao makuu ya polis ya mji wa Cinar, kilomita thelathini kusini mwa mji wa Diyarbakir, mji mkubwa wa kusini mashariki mwa Uturuki, unaokaliwa na wakurdi wengi nchini humo.

Watu wawili wameuawa katika mlipuko wa bomu lililotegwa ndani ya gari na wengine wanne, ikiwa ni pamoja na mtoto, wameuawa baada ya kuangukiwa na jengo lilio karibu na makao makuu ya polisi ya Cinar , ambapo wanaishi maafisa na familia zao, taarifa ya Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Diyarbakir imeripoti.

Wote waliouawa ni raia wa kawaida, mamlaka ya mkoa wa Diyarbakir imeeleza, na kuongeza kwamba askari polisi ni miongoni mwa waliojeruhiwa pia.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Ufaransa la AFP, jengo lwalikokua wakiishi askari polisi na familia zao limeanguka kutokana na mlipuko, makao makuu ya polisi na majengo mengine yanayozunguka eneo hilo yalipata hasara kubwa pia.

Baada ya mlipuko wa bomu lilotengwa ndani ya gari, watu walioonekana kama wapiganaji wa kundi la waasi la PKK, waliendelea na mashambulizi yao usiku kucha wakitumia bunguki za kurusha makombora, na kusababisha vikosi vya usalama kujibu.