UFARANSA-UGAIDI-MAUAJI-USALAMA

Mtu wa nane katika mashambulizi ya Paris atambuliwa

Ilichukua miezi miwili kwa wachunguzi ili kutoa jina la mtu wa tatu miongoni mwa watu waliohusika katika shambulio la kigaidi lililoendeshwa katika eneo la Saint-Denis, siku chache baada ya mashambulizi ya mjini Paris.

Saint-Denis, 18 novembre, la police sécurise les parages du lieu où l'assaut sera donné.
Saint-Denis, 18 novembre, la police sécurise les parages du lieu où l'assaut sera donné. REUTERS/Christian Hartmann
Matangazo ya kibiashara

Ilijulikana kuwa mtuhumiwa wa maandaalizi ya mashambulizi, Abdelhamid Abaaoud alihusika, pamoja na binamu yake, Hasna Ayt Boulhacene. Katika kundi hilo pia kulikuwa na Chakib Akrouh.

Chakib Akrouh, mwenye umri wa miaka 25, ni raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Morocco. Mwili wake ulikuwa katika hali mbaya kutokana na shambulio hilo, na uchunguzi wa vinasaba vya damu uliofanyika kwa mama yake ulisaidia kumtambua.

Chakib Akrouh alikua miongoni mwa kudi la magaidi walioendesha shambulio katika eneo la Saint-Denis. Miongoni mwa watu walikua wakiunda kundio hilo kuna wale walioendesha mashambulizi ya kujitoa mhanga katika maeneo ya 10 na 11 ya mji wa Paris. Katika gari lililotumiwa katika mashambulizi hayo walikuemo Abdelhamid Abaaoud na Brahim Abdeslam, ambaye alifariki dakika chache baadaye kwa kwa kujilipua mbele ya mgawaha mmoja, bila kusababisha athari yoyote.

Kwa sasa wanajulikana watu wa nane kati ya watu kumi ambao walishiriki katika mashambulizi yaliyowauawa watu 130 mjini Paris. Bilal Hadfi ni miongoni mwa washambuliaji waliojitoa mhanga mbele ya eneo la Stade de France. Katika eneo hilo kulionekana pasi mbili za kusafiria za Syria juu ya miili miwili ya wanachama wa kundi hilo la magaidi. Lakini ilidhihirika kuwa pasi hizo haizikua za halali, na majina yao au nchi wanakotoka havijajulikana.

Hatimaye kuna Salah Abdeslam. Yeye, anatuhumiwa kuwa aliambatana na kundi hili la magaidi katika eneo la Stade de France.Mtuhumiwa huyo mpaka sasa bad anatafutwa na polisi za Ulaya.