UTURUKI-WATUHUMIWA-SHERIA

Uturuki: watuhumiwa kumi washtakiwa kwa shambulio Istanbul

Askari polisi wa Uturuki akipiga doria katika eneo la kitalii la Sultanahmet, Istanbul, Januari 15, 2016.
Askari polisi wa Uturuki akipiga doria katika eneo la kitalii la Sultanahmet, Istanbul, Januari 15, 2016. AFP/AFP/

Mahakama mjini Istanbul imewashitaka na kuwafunga watuhumiwa kumi Jumapili hii jioni kwa kosa la "kuwa katika kundi la kigaidi", "kuhusika katika shambulio la kujitoa mhanga" Jumanne Januari 12 jijini Istanbul na kuuawa watalii kumi kutoka Ujerumani.

Matangazo ya kibiashara

Shambulio ambalo lilidaiwa kutekelezwa na kundi la Islamica State, shirika la habari Dogan, limearifu.

Watuhumiwa wengine sita ambao pia wamesikilizwa mbele ya majaji wataachiwa huru, Dagon imeongeza.

Jumla ya watu 16 wamefikishwa Jumapili hii asubuhi mbele ya mahakama hii, ambapo waendesha mashitaka waliomba watuhumiwa wote wahukumiwe kifungo jela.

Siku ya Alhamisi, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki, Ala Efkan, alisema kuwa watu saba kwa jumla wanaohusika katika shambulio hilo walikamatwa. Tangu wakati huo hakuna tangazo rasmi lililotolewa.

Mashambulizi ya siku ya Jumanne asubuhi yalilenga kundi la watalii kutoka Ujerumani mita mia moja kutoka Kanisa la St Sophia na Msikiti wa Blu, sehemu mbili muhimu zinazotembelewa na watu wengi katika mji huo mkubwa wa Uturuki.

Kwa mujibu wa serikali ya Uturuki, shambulio hilo lilitekelezwa na kijana mmoja wa Syria, mwenye umri wa miaka 28, aliyetambuliwa katika vyombo vya habari kama Nabil Fadli, ambaye, kwa mujibu wa Waziri Mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu ni "mwanachama" wa kundi la Islamic State (IS), na aliingia katikaardhi ya Uturuki kutoka Syria kama "mhamiaji" wa kawaida.

Watu kumi na saba pia walijeruhiwa katika shambulio hilo.

Tangu shambulio, liliodaiwa kutekelezwa na kundi al IS, ambalo liliua watu 103 mbele ya kituo cha treni mjini Ankara mwezi Oktoba 2015, polisi ya Uturuki imeongeza operesheni zake dhidi ya wanamgambo wa kundi la IS. Pia imeimarisha udhibiti na ukaguzi kwenye mipaka yake ili kuzuia zoezi la kusajili raia wa kigeni wanaojiunga na kundi la Islamic State nchini Syria.