IMF-LAGARDE

Christine Lagarde mgombea kwenye nafasi ya uongozi wa IMF

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Christine Lagarde.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Christine Lagarde. REUTERS/Stephen Jaffe/IMF Staff Photo/Pool

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Christine Lagarde, ambaye muhula wake unamalizika Julai 5, amesema Ijumaa hii kwamba atagombea kwa muhula mpya kama mkuu wa taasisi hiyo ya fedha duniani.

Matangazo ya kibiashara

MF imefungua mlango Alhamisi wiki hii kwa kutaka wagombea kuanza kuwasilisha fomu zao za kugombea na ina matumaini makubwa kwa ya kumteuwa kwa mara nyingine mwanamke huyo jasiri.

"Mimi ni mgombea kwa muhula mwengine", amesema Christine Lagarde kwenye runinga ya Ufaransa France 2. "Nilipata heshima tangu mwanzo wa utaratibu uungaji mkono wa Ufaransa, Uingereza, Ujerumani, China na Korea ".

Kuhusu msimamo wa Marekani, ilieleza hivi karibuni kumuunga mkono Makamu wake wa Rais Joe Biden.

"Kama wanachama wote wa taasisi hii wanataka niendelea, sintosita kugombea", Lagarde amesema.