UINGEREZA-URUSI-USHIRIKIANO

Putin ahusishwa katika kesi ya mauaji ya Litvinenko

Rais wa Urusi Vladmir Putin
Rais wa Urusi Vladmir Putin Reuters

Utawala wa Moscow umeeleza kuchukizwa na taarifa ya jopo la uchunguzi nchini Uingereza kuitaja nchi hiyo na rais Vladmir Putini kuhusika katika njama na kutekeleza mauaji dhidi ya jasusi wa zamani wa nchi hiyo, Alexander Litvinenko aliyeuawa kwa sumu jijini London.

Matangazo ya kibiashara

Urusi inasema ripoti ya uchunguzu kuhusu kifo cha Litvinenko haina nia njema na inalenga kuzorotesha uhusiano uliopo kati ya nchi hizo mbili, ambapo inahoji uhalali wa ripoti hiyo kumuhusisha rais Putini.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza,Theresa May, amesema ripoti hii itachukuliwa kwa umakini na serikali itatangaza hatua zaidi.

Katika hatua nyingine, saa chache baada ya kuitwa kutoa maelezo katika izara ya Mambo ya Nje ya Uingereza, balozi wa Urusi nchini humo, Alexander Yakovenko amesema hawakubalini na ripoti huyo alioiita ya kutengenezwa.

Uingereza inataka raia wawili wa Urusi, Andrei Lugovoi na Dmitro Kovtun kupelekwa nchini humo kujibu mashtaka ya tuhuma za mauaji yanayowakabili, huku Urusi ikikataa ombi la kuwasafirisha.