URENO-UCHAGUZI

Ureno: Rebelo de Sousa ashinda katika duru ya kwanza ya uchauguzi

Mgombea kwa tiketi ya chama cha Conservaitve Marcelo Rebelo de Sousa alikua akipewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi wa urais nchini Ureno.
Mgombea kwa tiketi ya chama cha Conservaitve Marcelo Rebelo de Sousa alikua akipewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi wa urais nchini Ureno. REUTERS/Rafael Marchante

Mgombea kwa tiketi ya chama cha Conservative Marcelo Rebelo de Sousa, mwenye umri wa miaka 67, ameshinda Jumapili hii uchaguzi wa urais katika duru ya kwanza nchini Ureno, kulingana na matokeo rasmi kutoka karibu 97% ya vituo vua kupigia kura.

Matangazo ya kibiashara

Profesa huyo wa sheria, na mtu muhimu kwa maoni mbalimbali kwenye runinga kwa miaka zaidi ya kumi na tano iliyopita, amepata 52.78% ya kura, akimshinda mgombea binafsi kutoka mrengo wa kushoto Antonio Sampaio da Novoa, ambayea mepata 22.17 ya kura, kulingana na matokeo ya muda.

Marisa Matias, mgombea wa mrengo wa kushoto, wenye uhusiano na chama cha SYRIZA nchini Ugiriki, ameshangaza wengi kwa kuchukua nafasi ya tatu, bada ya kupata 10% ya kura, akimbele ya Waziri wa zamani kutoka chama cha Kisoshalisti Maria de Belem Roseira, ambaye amepata 4.27% ya kura pamoja na mgombea wa Kikomunisti Edgar Silva (3.87%).

Bwa Rebelo de Sousa, kiongozi wa zamani wa chama cha Democratic Party cha mrengo wa katikati kulia), anamrithi kiongozi mwingine kutoka cgama cha Conservative Anibal Cavaco Silva, ambaye anamaliza muhula wake wa pili mfululizo, akiwa na umri wa miaka 76, sawa na muhula wa mwisho unaoruhusiwa na Katiba ya Ureno.

Idadi ya watu ambao wamejizuia kupiga kura imepungua, na kufikia kati ya 52.1%, baada ya rekodi iliyofikia 53.5% katika uchaguzi wa rais uliopita, mwaka 2011. Kama rais wa nchi ya Ureno hana mamlaka yoyote katika serikali, ana nguvu zingine ambazo ni pamoja na: kuvunja Bunge, suala kuu la kampeni ambayo haikuwavutia wengi.