EU-UKAGUZI-USALAMA

Kuelekea kudumisha udhibiti wa mipaka katika eneo la Schengen

Askari polisi wa Denmark katika mpaka na Ujerumani.
Askari polisi wa Denmark katika mpaka na Ujerumani. REUTERS/Claus Fisker/Scanpix Denmark

Mawaziri wa mambo ya ndani wa Umoja wa Ulaya, waliokutana Jumatatu hii katika mji wa Amsterdam, waameomba Tume ya Ulaya kuandaa hatua za kisheria kwa ajili ya kuruhusu kudumisha, ikiwa inahitajika kwa miaka miwili, udhibiti wa mipaka uliowekwa na baadhi ya nchi wanachama wa eneo la Schengen dhidi ya mgogoro wa uhamiaji

Matangazo ya kibiashara

"Kwa sasa, hatua hizi za muda zinaweza kuchukuliwa tu kwa miezi sita. Lakini ongezeko la wakimbizi, ambalo lilipelekea baadhi ya nchi wanachama kuchukua hatua hizi katika ngazi ya kitaifa, halikukoma", Waziri wa Uhamiaji wa Uholanzi, Klaas Dijkhoff, amesema katika mkutano na waandishi wa habari.

"Mataifa wanachama wameomba Tume kuandaa misingi ya kisheria na kutekeleza kwa muendelezo wa hatua za muda (kufanya ukaguzi kwenye mipaka), kwa mujibu wa Ibara ya 26 ya sheria ya Schengen", Klass Dijkhoff ameongeza.

Eneo la Schengen la uhuru wa kutmbea barani Ulaya linaundwa na mataifa 26, ambapo 22 ni wanachama wa Umoja wa Ulaya. Nchi sita zimeamua kwa muda kurejesha udhibiti katika mipaka yao. Nchi hizi ni pamoja na Ujerumani, Austria, Ufaransa, Denmark, Sweden na Norway. Udhibiti huu unaweza kubaki hadi Mei

Kulingana na kanuni za Schengen, ukaguzi wa muda katika mipaka ya ndani inaweza unaweza kuongezwa kwa kipindi kisichozidi miaka miwili.