UFARANSA-INDIA-MKATABA

Ufaransa na India zahitimisha makubaliano kuhusu Rafale

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi (kulia) na Rais François Hollande, Januari 25, 2016 mjini New Delhi.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi (kulia) na Rais François Hollande, Januari 25, 2016 mjini New Delhi. STEPHANE DE SAKUTIN/AFP

Ufaransa na India wamekubaliana Jumanne kwa kulipa jeshi la India ndege kubwa 36 za kivita (Rafale) za Ufaransa lakini bila kukubaliana juu ya suala la fedha, na wamekubaliana kuimarisha ushirikiano wao katika suala la ulinzi kufuatia tishio la kigaidi.

Matangazo ya kibiashara

Mashaka juu ya kurasimisha mkataba kuhusu ndege kubwa za kivita (Rafale) umezungumziwa katika siku ya pili ya ziara ya Rais François Hollande nchini India, katika taarifa ya pamoja na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi na Rais wa Ufaransa. "Tumeafikiana makubaliano baina ya serikali kuhusu ununuzi wa ndege kubwa 36 za kivita (Rafale), isipokuwa kwa masuala ya fedha", amesema Bw Modi.

Akipongeza "hatua kubwa kwa India kupata" mitambo mikubwa kutoka kampuni ya vifaa vya ndege Dassault Aviation, Bw Hollande amehakikisha kwamba "masuala ya fedha" yatakuwa "yametatuliwa katika siku zijazo."

Katika hali halisi kampuni ya Dassault Aviation imesema katika taarifa yake kwamba, kanuni hii itakua imefanikiwa ndani ya wiki nne.

"Makubaliano hayakutiliwa saini lakini yamethibitishwa, ina maana kwamba mazungumzo yamemalizika na kinachobaki ni suala la bei na wakati wa kuagiza ndege hizo", wamesema kwa upande wao wasaidizi wa Rais wa Ufaransa.

Kiwango cha pesa cha mkataba huo ambao umekua chini ya majadiliano kwa miaka kadhaa kati ya Ufaransa na India, kiinakadiriwa kuwa sawa na euro bilioni kadhaa.

Hitimisho la mkataba huu unakuja masaa kadhaa baada ya kurushwa hewani kwa video ya kundi la Islamic State ikionyesha washambuliaji wake tisa jinsi walivyotekeleza mashambulizi yaliogharimu maisha ya watu 130 Novemba 13 mjini Paris.