UFARANSA-INDIA-MKATABA

India: Hollande amaliza ziara yake kwa gwaride la Republic Day

Kikosi cha wanajeshi wa ulinzi wa Reli cha jeshi la India katika gwaride la Repulic Day, Januari 26, 2016 New Delhi.
Kikosi cha wanajeshi wa ulinzi wa Reli cha jeshi la India katika gwaride la Repulic Day, Januari 26, 2016 New Delhi. PRAKASH SINGH/AFP

Rais wa Ufaransa François Hollande, amehudhuriwa Jumanne hii gwaride la Republic Day, mazoezi yanayoonyesha nguvu za jeshi la India na utamaduni wake tofauti, kwa siku ya mwisho ya ziara yake nchini India.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mara ya tano, Rais wa Ufaransa amekuwa mgeni rasmi katika gwaride hilo, rekodi ambayo inaadhimisha kumbukumbu ya Katiba ya India iliyotangazwa mwaka 1950.

Kwa jambo lisilokuwa la kawaida, kambi ya 35 ya wanajeshi wa nchi kavu wa Ufaransa na wanamuziki wa nyimbo za kikosi cha wanajeshi wa nchi kavu wamealikwa na kuwekwa kwenye nafasi ya mbele katika gwaride hilo, huku wakifuatiwa na magari manne ya maveterani wa India.

Hakuna askari wa kigeni ambao mpaka sasa wameshiriki gwaride hili la jeshi la India linalofanyika kila Januari 26.

Gwaride hili limeanzia kutoka Ikulu ya Rais na limeendelea kwenye barabara kuu (Rajpath) inayopita katikati mwa mji mkuu na kuendelea hadi India Gate, ambapo kulijengwa mnara wa kumbukumbu wa askari wasiojulikana.

Gwaride hili lililodumu saa moja na nusu limefanyika chini ya ulinzi mkali wa polisi. Maafisa wa usalama 50,000 wametumwa ili kutoa ulinzi wa mji mkuu, kwa mujibu wa msemaji wa polisi.

François Hollande na Waziri Mkuu Narendra Modi wamefuata gwaride hilo wakiwa nyuma ya kioo ambacho si rahisi kuvunjwa na risasi. India na Ufaransa ni nchi ambazo zinakabiliwa na tishio la mashambulizi mapya.