UFARANSA-MAANDAMANO-MGOMO

Mgomo wa madereva wa Teksi Ile-de-France: watu 20 wakamatwa

Hali halisi inayojiri Ufaransa Jumanee hii, Januari 26, hasa katika eneo la Porte Maillot wakati wa maandamano ya madereva wa teksi mjini Paris.
Hali halisi inayojiri Ufaransa Jumanee hii, Januari 26, hasa katika eneo la Porte Maillot wakati wa maandamano ya madereva wa teksi mjini Paris. AFP/AFP

Watu ishirini wamekamatwa Jumanne hii asubuhi katika jimbo la Ile-de-France wakati wa maandamano ya madereva wa teksi dhidi ya ushindani wa magari ya usafiri yenye madereva (VTC), chanzo kutoka makao makuu ya polisi kimebaini.

Matangazo ya kibiashara

Kwa jumla, waandamanaji 19 wamekamatwa katika eneo la Porte Maillot, baada ya eneo hilo kuzuiliwa, wakati ambapo dereva mmoja alitumia nguvu za kupita kiasi na kugonga vizuizi viliyokuwa vimewekwa barabarani na hivyo kumdondosha mmoja kati ya waandamanaji. Dereva huyo amekamatwa na kwa sasa anazuiliwa katika majengo ya polisi kwenye uwanja wa ndege wa Orly.

Hali ya taharuki imetanda katika sekta ya umma na ile ya watu binafsi Jumanne hii, nchini kote Ufaransa dhidi ya mageuzi ya katika skta ya uchukuzi (VTC): Mgomo huo unnaingiliana na maandamano ya wafanyakazi wa serikali.

Kwa mujibu wa makao makuu ya polisi, teksi 1,200 zimeshuhudiwa katika maeneo mbalimbali ya maandamano, hasa katika mji wa Orly waandamanaji kadhaa wamezingira eneo la A 106

Taksi pia zimekuwepo katika uwanja wa ndege wa Roissy.

Wakati huo huo, katika ekta ya umma (wafanyakazi milioni 5.6), maandamano kati ya 110 na 120 yamepangwa kufanyika nchini Ufaransa, maandamano ambayo wanatazamiwa kujiunga walimu pamoja na wafanyakazi wengine katika sekta mbalimbali kama vile Afya, Fedha,...