IRAN-UFARANSA-USHIRIKIANO

Iran: makubaliano ya kupata ndege 118 aina ya Airbus

Waziri wa mambo ya Nje wa Ufaransa, Laurent Fabius (kulia) na mwenzake wa Iran Mohammad Javad Zarif (kushoto) wakiweka saini kwenye mikataba chini ya uangalizi wa marais wa Iran Hassan Rouhani na Ufaransa Francois Hollande, katika Elysée mjini Paris.
Waziri wa mambo ya Nje wa Ufaransa, Laurent Fabius (kulia) na mwenzake wa Iran Mohammad Javad Zarif (kushoto) wakiweka saini kwenye mikataba chini ya uangalizi wa marais wa Iran Hassan Rouhani na Ufaransa Francois Hollande, katika Elysée mjini Paris. AFP/AFP

Iran imejikubalisha kulipa nusu ya pesa ya malipo katika upatikanaji wa ndege 118, mbele ya kampuni inayotengeneza ndege aina ya Airbus barani Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Mkataba huo umefanyika wakati wa ziara ya Rais wa Iran Hassan Rouhani mjini Paris.

Ndege hizo zitanunuliwa Dola bilioni 25, kama alivyoshuhudia mwandishi wa habari wa shirika la habari la Ufaransa AFP.

Tangazo hili limetolewa wakati wa sherehe katika Ikulu ya Elysée, akiwepo Rais Ufaransa François Hollande. Huu ni mkataba wa kiitifaki na si mkataba wa moja kwa moja kutokana na kuondolewa kwa sehemu ya vikwazo dhidi ya Iran.