UFARANSA-WAKIMBIZI

Calais: mgogoro wa wakimbizi wachukua sura mpya

Wairani 3, ambao wameshona mdomo yao, wakipinga dhidi kuvunjwa kambi ya "Jungle" katika moka wa Calais, Machi 3, 2016.
Wairani 3, ambao wameshona mdomo yao, wakipinga dhidi kuvunjwa kambi ya "Jungle" katika moka wa Calais, Machi 3, 2016. PHILIPPE HUGUEN/AFP

Mgogoro wa wahamiaji katika mkoa wa Calais, Alhamisi hii, umechukua sura mpya, kwa ishara iliyofanywa hadharani na kundi la wakimbizi kutoka Iran ambao wameshona midomo yao katika kambi ya "Jungle", kwa masaa kadhaa baada ya juhudi kama hizo za baadhi ya raia wenzao.

Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo, lililodumu muda wa dakika kumi, lilitokea katikati ya umati wa watu, mbele ya wapiga picha, kwenye "ukumbi" wa kibanda, mbele ya ofisi ya shirika la Madaktari Wasiokuwa na Mipaka (MSF) katika eneo la kusini mwa kambi inayotazamiwa kuhamishwa. Wairani tisa walikua wameshona midomo yao au walikuwa katika mchakato wa kushona midomo yao kwa sindano na uzi, bila kujua kama baadhi yao walikuwa tayari wameshona midomo ya siku moja kabla.

Kundi hili linaloundwa tu na wanaume, ambao walikuwa karibu wote wamejificha nyuso zao, ambazo zilifunikwa na mitandio iliokua imetobolewa kwenye sehemu ya macho. Mmoja wao, mwenye umri wa miaka arobaini, amekua akipiga kelele.

Kwenye mabango waliokua nayo kulikua kumeandikwa "Will you listen now?" ("Je, mtatusikiliza sasa?"). Taarifa nyingine zinasema kuwa walikua katika mgomo wa wa kususia chakula. Wakati huo huo kibanda kimoja kilichomwa moto.

Kisha waliandamana kwa muda wa dakika kumi kabla ya kutawanyika mbele ya vikosi vya usalama.

siku moja baadaye, Wairan 8, kwa mujibu wa mashirika mawili ya kusaidia wahamiaji, Wairan wawili kwa mujibu wa mamlaka ya mkoa, walikua tayari wameshona midomo yao. Walifanya hivyo "kwa sababu kibanda chao kimeteketea kwa moto," François Guennoc, wa chirika la kusaidia wahamiaji la Auberge des migrants, amesema.

Mgogoro huu utajadiliwa Ijumaa hii kwenye Ikulu ya Elysée na Rais wa Ufaransa François Hollande ambaye, mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani Bernard Cazeneuve, atampokea Meya wa mji wa Calais, Natacha Bouchard, pamoja na mwenyekiti mkoa Xavier Bertrand na madiwani wawili waliochaguliwa katika mkoa huo.

Wakati huo huo London imeahidi kutoa milioni 22 ya misaada ya ziada kwa Ufaransa kwa kusaidia kusimamia hali ya wakimbizi katika mkoa wa Calais.