UBELGIJI-UFARANSA-USALAMA-UGAIDI

Polisi ya Ubelgiji yanyooshewa kidole

Askari polisi wa Ubelgiji wakipiga doria katika kata ya Molenbeek, Desemba 30, 2015.
Askari polisi wa Ubelgiji wakipiga doria katika kata ya Molenbeek, Desemba 30, 2015. AFP/Belga/AFP

Maswali mengi yameibuka kuhusu uwajibikaji wa polisi ya Ubelgiji ambayo inatuhumiwa kupuzia mwezi Julai 2014 taarifa muhimu kuhusu ndugu wawili waitwao Abdeslam, walioendesha mashambulizi mjini Paris.

Matangazo ya kibiashara

Suala hililimekua gumzo kwenye vyombo vya habari vya Ubelgiji, lakini mamlaka ya nchi hiyo inasubiri uamuzi wa uchunguzi wa "Polisi" ili iweze kuamua.

"Kama tungelijua kwamba hakukuwa na uwajibikaji kwa upande wa polisi, ningelishirikiana nanyi kwa kusahihisha hili," amesema Alhamisi hii Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ubelgiji, Jan Jambon, alipokua akihojiwa katika kikao cha Bunge.

Waziri ameeleza kwamba bado anasubiri "Kamati P", mamlaka huru inayohusika na ukaguzi wa polisi, kuhitimisha kazi iliopewa. Kamati hii itawasilisha Jumatatu, Machi 7 kwa kundi dogo la Wabunge watakao kutana katika kikao cha faragha, ripoti ya muda mfupi kuhusu mashambulizi ya Novemba 13.

"Nimeisoma ripoti hiyona, lakini hawaelezi chochote kuhusu" ushahidi unaotolewa na magazeti mbalimbali, Bw Jambon ameongeza. "Nina wazo kwamba Kamati P pia itatathmini baadaye taarifa hii, hivyo basi tusubir ripoti zao," Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ubelgiji ameomba.

"Mamlaka inayohusika na ukaguzi wa polisi" inachunguza taarifa ya Julai 2014 kuhusu uwezekano wa msimamo mkali wa ndugu wawili Salah na Brahim Abdeslam, wawili kati ya wahusika wa mashambulizi ya Paris, vyombo vya habari vya Ubelgiji vimearifu Alhamisi hii.

Usiku wa Julai 10 kuamkia 11, 2014, miezi kumi na sita kabla ya mashambulizi hayo yaliowaua watu 130, afisa wa polisi alipokea simu kutoka kwa "ndugu wa familia ya Abdeslam ( mkazi wa kata moja ya mji wa Brussels) ya Molenbeek, ambaye alimpasha habari zinazohusiana na watu hao hatari" kulingana na magazeti ya kila siku ya La Dernière Heure (" DH ") na Het Laatste Nieuws.

Mtu huyo alieleza kuwa ndugu hao wawili ni watu wenye msimamo mkali wa kidini na walikua na mpango wa kusafiri nchini Syria, na walikuwa "chini ya ushawishi" wa mwanajihadi wa kata ya Molenbeek Abdelhamid Abaaoud (alieuawa wakati wa majibizano ya risasi na pilisi katika eneo la Saint-Denis) na walikuwa na "mipango ya mashambulizi," kwa mujibu wa chanzo hicho.

Afisa huyo wa polisi, ambaye wakati huo alikuwa katika "likizo ya ugonjwa", anadai kuwa aliwasilisha usiku huo huo taarifa kwa wenzake wa kitengo cha polisi ya kupambana na ugaidi (DR3), magazeti hayo yameeleza. Afisa huyo amesikilizwa na Kamati P, gazeti la kila siku la Laatste Nieuws limearifu.

Ikihojiwa Jumanne wiki hii juu ya makala yakiochapishwa na magazeti hayo katika mwelekeo huo huo, Ofisi ya mashitaka ilipuuzia umuhimu wa taarifa hizo iliokuwa nazo wakati huo, na kutaja kuwa kutokua "sahihi" matokeo ya utafiti yanayoonyesha kwamba "mashambulizi ya Paris yangeliepukika tangu Ubelgiji".