UKRAINE-UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi Mashariki mwa Ukraine kufanyika kabla ya mwezi Julai

Kutoka kushoto kwenda kulia, mawaziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov, wa Ukraine Pavlo Klimkin, wa Ufaransa Jean-Marc Ayrault na wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier, Machi 3, Quai d'Orsay.
Kutoka kushoto kwenda kulia, mawaziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov, wa Ukraine Pavlo Klimkin, wa Ufaransa Jean-Marc Ayrault na wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier, Machi 3, Quai d'Orsay. REUTERS/Jacky Naegelen

Uchaguzi wa serikali za mitaa katika eneo la Donbass lililojitenga, mashariki mwa Ukraine unatazamiwa kufanyika kabla ya mwezi Julai: ni dhamira ya mawaziri wa Mambo ya Kgeni wa Ufaransa, Ujerumani, Ukraine na Urusi.

Matangazo ya kibiashara

Mawaziri hao waliokutana Alhamisi hii jioni Machi 3 katika jengo la Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Ufaransa (Quai d'Orsay) mjini Paris, walijaribu kusonga mbele kuhusu pointi kadhaa za mikataba ya Minsk, ambayo imeshindwa kutekelezwa na kuweka kalenda ya shughuli zao. Lakini mchakato wa amani bado ni tete.

Juhudi za Paris na Berlin kwa kufufua mazungumzo yenye lengo la kukomesha mgogoro mashariki mwa Ukraine yameingiliwa na mashaka juu ya ukosefu wa ahadi madhubuti ya Kiev na Moscow, licha ya tarehe ya mwisho iliyotolewa Alhamisi hii kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa ambao umetajwa kuwa muhimu.

Baada ya mkutano wa uliodumu masaa kadhaa mjini Paris kati ya mawaziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Ujerumani, Ukraine na Urusi, Waziri wa mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Marc Ayrault alisema kuwa uchaguzi katika ukanda unaoungwa mkono na Urusi wa Donbass unapaswa kufanyika mwezi Julai, uchaguzi ambao Paris na Berlin umekua ukiomba serikali ya Kiev kwa miezi kadhaa bila mafanikio.

"Tulisisitiza umuhimu wa kupitishwa kwa sheria ya uchaguzi kwa kufanyika uchaguzi wa serikali za mitaa kabla ya mwisho wa nusu ya kwanza ya mwaka 2016," Bw Ayrault amewaambia waandishi wa habari. "Tunahitaji kuhakikisha usalama wa maandalizi ya uchaguzi, tunahitaji usalama katika maeneo ambapo uchaguzi utafanyika," hata hivyo amemtuliza mwenzake wa Ukraine Pavlo Klimkin, akitaja kuwa mkutano wa Alhamisi ulikabiliwa na changamoto nyingi na hivyo kushindwa kuendelea.

Kama nchi za Magharibi zinaona kuwa uchaguzi katika eneo la mashariki linalokaliwa na waasi ni ufunguzi kwa kuunganisha eneo hilo katika siasa za Ukraine, Kiev inahofia kwamba Urusi, inayotuhumiwa kuyasaidia kijeshi maeno yaliojitenga, inatumia fursa hiyo ili kudhoofisha hali ya usalama katika eneo nzima la Jamhuri ya Urusi ya zamani.