EU-UTURUKI-WAHAMIAJI

EU yatoa muda wa siku kumi kukamilisha makubaliano na Ankara

Waziri Mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu katika mkutano na waandishi wa habari aada ya mkutano na Umoja wa Ulaya, Brussels.
Waziri Mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu katika mkutano na waandishi wa habari aada ya mkutano na Umoja wa Ulaya, Brussels. REUTERS/Yves Herman

Umoja wa Ulaya umetoa siku 10 kukamilisha makubaliano mapya na Ankara yanayopania "kukabiliana" na ongezeko la wahamiaji wanaoingia Ulaya, ikiwa ni pamoja na pendekezo la kuwarejesha nchini Uturuki wahamiaji wote wanaovuka bahari ya Aegean, ikiwa ni pamoja na wakimbizi wa Syria.

Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu mpya kati ya viongozi wa nchi 28 na Uturuki, uliomalizika usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne baada ya majadiliano, umetoa ahadi ya majadiliano muhimu yaliopangwa kufanyika tarehe 17 na 18 mwezi Machi mjini Brussels.

"Muda wa uhamiaji haramu barani Ulaya umekamilika", Rais wa Baraza la Ulaya Donald Tusk amepongeza, licha ya ukosefu wa makubaliano ya jumla baada ya zaidi ya saa 12 ya mkutano.

Ankara imeshangaza wengi ikitoa mapendekezo mapya, yaliopendekezwa na Ujerumani pamoja na Tume ya Ulaya,kwa mujibu wa baadhi ya washiriki - lakini pia mahitaji mapya mbele ya mataifa ya Ulaya kwa lengo la kutafuta mno ufumbuzi wa mgogoro wa uhamiaji.

Uturuki imeomba Umoja wa Ulaya Euro bilioni tatu za msaada wa ziada, ili kuwapokea na kuwahudumia katika ardhi yake wakimbizi wa Syria, ambao wamefikia (milioni 2.7 kwa sasa).

Pia Uturuki imeahidi kwa kiasi kikubwa kuongeza ushirikiano wake katika mgogoro wa wahamiaji ili kukabiliana na ongezeko la wahamiaji, Spika wa Bunge la Ulaya Martin Schulz amesema Jumatatu hii.

"Fedha hizi za ziada zitahitaji taratibu za bajeti za ziada. Bunge la Ulaya likotayari kuharakisha taratibu," Schulz amesemakatika mkutano wa kilele wa EU-Uturuki mjini Brussels, ambapo Ankara imeonekana tayari kukubali kurudi kwa wahamiaji wengi, ikiwa ni pamoja na wakimbizi wa Syria.

Umoja wa Ulaya tayari umekubali kuisaidia Uturuki hadi kitita cha Euro bilioni tatu kwa ajili ya miradi ya kukuza ushirikiano wa wakimbizi milioni 2.7 wa Syria katika ardhi ya Uturuki, kwa elimu ya watoto katika lugha ya Kiarabu au kuwapatishia ajira kwa mfano, kama sehemu ya mpango wa utekelezaji wa pamoja uliosainiwa mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka 2015.

Lakini mpango ni mgumo kueleza iwapo utapelekea kushuka kwa kiasi kikubwa kwa kuwasili kwa wakimbizi kwenye pwani za Ugiriki wakitokea Uturuki. Jumapili hii jioni, Ankara imetoa mfululizo wa mapendekezo, ikiahidi kuwachukua, kuanzia tarehe 1 Juni, wahamiaji wa kiuchumi ambao iliwaacha waingiye Ulaya, ili iweze kuwarejesha katika nchi zao, lakini pia wakimbizi wa Syria.

Kwa upande wake, Umoja wa Ulaya imejikubalisha kuwezesha mifumo ya kisheria ya wakimbizi wa Syria katika umoja huo, moja kwa moja kutoka Uturuki, kwa idadi kubwa.

Uturuki inahitaji mambo mengine muhimu: pia inataka viza ya bure kwa raia wa Uturuki ianze kutekelezwa kabla ya mwisho wa mwezi Juni na inataka mazungumzo ya kujiunga na umoja wa Ulaya, yaliosimama kwa zaidi ya muongo mmoja, yaanzishwe upya haraka iwezekanavyo kutokana na ufunguzi wa sura mpya.