UFARANSA-AJIRA

Ufaransa: Hollande akubali kuifanyia marekebisho sheria ya kazi

Rais Francois Hollande akiwasili Venice kwa ajili ya mkutano kati ya  Italia na Ufaransa, Machi 8, 2016.
Rais Francois Hollande akiwasili Venice kwa ajili ya mkutano kati ya Italia na Ufaransa, Machi 8, 2016. AFP

Alhamisi hii, François Hollande ametupilia mbali kuondolewa kwa muswada wa sheria ya kazi, kwa sababu bado haujawasilishwa, lakini amekiri kwamba kuna uwezekano "muhimu" muswada huo ufanyiwe "marekebisho" na kusisitiza kuwa "CDI inapaswa kuwa njia ya kawaida ya kujiunga na makampuni mbaimbali. "

Matangazo ya kibiashara

"Inaandaliwa nakala (...) ambayo bado haijafahamika (...) itawasilishwa mbele ya Baraza la Mawaziri tarehe 24 Machi, ni kwa nakala hii ambapo Bunge litachukua uamuzi. Wazo si kuondoa kile ambacho bado hakijapitishwa, au kuwasilishwa ", Rais Hollande amesema wakati alipotembelea Alhamisi hii kampuni moja mjini Seine-et-Marne, ziara ambayo imefuatiwa na mazungumzo kati ya kiongozi huyo na wafanyakazi.

"Sheria inaweza kuboreshwa, kuna uwezekano wa kutoa ufafanuzi, marekebisho yanayotakiwa kufanyika ikilinganishwa na kile ambacho kinaweza kuwa mstari wa kwanza," Rais wa Ufaransa alisema.

"Kama mashauriano yamefanyika kwa ombi langu, ni kutaka kuleta ufafanuzi , maelezo yote, kuondoa wasiwasi, kuboresha zaidi kifaa hiki kwa kuzingatia yaliomo, kwa kuwa na matumaini," Rais Hollande amesisitiza.

"Matumaini, ni kwamba kuna ajira nyingi katika nchi yetu, ajira nyingi na zaidi ya vijana wanajiunga na CDI", Rais hollande ameongeza.

Alipoulizwa kuhusu kodi ya CDD, amejibu: "kutoza CDD, siyo katika nakala ya leo."

"Tunapaswa kushughulikia matatizo," amerejelea Hollande. Vijana, "ilikuwa kipaumbele changu na hakitobadilika," amesema. "Mpaka mwisho wa muhula wangu wa miaka mitano, vijana watapata, kama ikiwezekana, rasilimali ambazo zitakuwepo kwa ajili yao, kwa sababu wao ni mustakabali wetu."