UTURUKI-ERDOGAN-SHERIA

Rais Erdogan akosoa Mahakama ya Katiba ya Uturuki

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, wakati wa hotuba yake katika Ikulu ya rais mjini Ankara, Novemba 26, mwaka 2015.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, wakati wa hotuba yake katika Ikulu ya rais mjini Ankara, Novemba 26, mwaka 2015. REUTERS/Umit Bektas

Uamuzi wa Mahakama ya Katiba ya kuagiza kuachiliwa huru kwa waandishi wa habari wawili wanaofanya kazi katika gazeti la upinzani ni uamuzi dhidi ya Uturuki na watu wake, amesema Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan Ijumaa hii.

Matangazo ya kibiashara

Mahakama Kuu nchini Uturuki iliamuru mwezi uliopita kuachiliwa huru kwa Can Dundar na Erdem Gül, mhariri na mkuu wa ofisi ya gazeti la Cumhuriyet mjini Ankara, ikibaini kwamba kuzuiliwa kwao ilikuwa kinyume cha sheria.

Waandishi wa habari wawili walikamatwa mwezi Novemba kutokana na kuchapisha habari ambazo mamlaka ya Uturuki imezitaja kuwahaziendani na na usalama wa nchi. Wanahabari hao walishtumiwa kusaidia kundi la kigaidi linalotumia silaha.

"Taasisi hii, kwa ushirikiano wa mwenyekiti wake na baadhi ya majaji wake haikusita kuchukua uamuzi ambao unakwenda kinyume na nchi na watu wake, kuhusu tatizo ambalo ni mfano halisi wa moja ya mashambulizi muhimu ya hivi karibuni dhidi ya Uturuki," Erdogan amesema katika mkutano wa hadhara katika mji wa Burdur, kusini-magharibi mwa Uturuki.

"Natumaini kwamba Mahakama ya Katiba haitoendesha juhudi mpya za aina hii ambazo zingeweza kusababisha hoja ya kuwepo kwake na uhalali wake," ameongeza Rais Erdogan katika hotuba iliyorushwa hewani kwenye runinga ya serikali.

Gazeti la Cumhuriyet ililichapisha mwezi Mei picha, video na kutoa taarifa inayoonyesha maafisa wa Idara ya Ujasusi ya Uturuki wakisafirishasilaha katika malori nchini Syria mwaka 2014. Rais Erdogan alibaini wakati huo kwamba taarifa hiyo ni sehemu ya mradi wenye lengo la kudhoofisha Uturuki, jambo ambalo hawezi kusamehe, alisema Rais Erdogan.