UTURUKI-SHAMBULIO-USALAMA

Uturuki: watu zaidi ya 25 wauawa, 75 kujeruhiwa katika shambulio Ankara

Polisi kwenye teneo la shambulizi, Machi 13, 2016  Ankara, Uturuki.
Polisi kwenye teneo la shambulizi, Machi 13, 2016 Ankara, Uturuki. AFP/AFP

Watu wasiopungua 27 wameuawa na wengine 75 kujeruhiwa katika shambulio la bomu lililotegwa ndani ya gari Jumapili hii jioni katikati mwa mji waAnkara, wiki zaidi ya tatu baada ya mashambulizi ya kujitoa mhanga yaliogharimu maisha ya watu 29 katika mji mkuu wa Uturuki.

Matangazo ya kibiashara

"Mlipuko huo umesababishwa na gari iliyojaa vilipuzi karibu na eneo la Kizilay," ofisi ya mkuu wa mji wa Ankara imesema katika taarifa.

Mlipuko huo ulitokea saa 12:45 jioni saa za Uturuki (sawa na saa 10:45 saa a kimataifa) katika eneo hilo linalotembelewa na watu wengi katikati mwa mji mkuu wa Uturuki, ambao una maduka mengi, na barabara makuu yanayotumiwa na mabasi na ambapo kuna kituo cha treni ya mwendo wa kasi.

Magari mengi ya wagonjwa yametumwa eneo la shambulizi, kulingana na picha za mwanzo zilizorushwa kwenye vyombo vya habari vya Uturuki, ambavyo pia vimeonyesha mabasi kadhaa yalioteketezwa kwa moto.

Ishara ya vurugu ya mlipuko huo, watu wasiopungua 23 wakufa papo hapo na wengine wamefariki wakati wakisafirishwa katika hospitalini, kwa mujibu wa runinga ya CNN-Turk.

Watu waliojeruhiwa wanapatishiwa matibabu katika hospitali kumi za mji mkuu, "kumi kati yao " wako katika hali mbaya, chanzo kitabibu kililiambia shirika la habrai la Ufaransa la AFP.

Hakuna kundi ambalo limeshadai shambulizi hili

Polisi ya Uturuki kuwa imetuma idadi kubwa ya askari polisi ili kuzuia njia zinazoelekea eno la tukio, huku helikopta zikiwa ndio zinazunguuka juu ya anga ya eneo hilo, mpiga picha wa AFP ameshuhudia.

Februari 17, shambulio la kujitoa mhanga la bomu lililotegwa ndani ya gari, ambalo lilidaiwa kutekelezwa na kundi la wapiganaji la PKK, lililolenga magari yaliokua yakiwasafirisha wanajeshi liliwaua watu 29.