EU-UTURUKI-WAHAMIAJI

Mgogoro wa wahamiaji: tofauti zasalia kubwa kati ya nchi 28 za EU

Viongozi wa Ufaransa Hollande, Ugiriki Alexis Tsipras na Ujerumani Angela Merkel wamejaribu kuendeleza mkataba kwa kutafutia suluhu mgogoro wa wahamiaji katika bara la Ulaya, pamoja na nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Ulaya.
Viongozi wa Ufaransa Hollande, Ugiriki Alexis Tsipras na Ujerumani Angela Merkel wamejaribu kuendeleza mkataba kwa kutafutia suluhu mgogoro wa wahamiaji katika bara la Ulaya, pamoja na nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Ulaya. REUTERS/Stephane de Sakutin/Pool

Alhamisi hii, MAchi 17, nchi 28 wanachama wa Umoja wa Ulaya wamefanya mazungumzo na Uturuki. Lengo ni kukamilisha maelezo ya mkataba unaotakiwa kuzuia wimbi la wahamiaji wanaoingia Ulaya. Mkataba ambao maudhui yake yalielezwa wiki mbili zilizopita.

Matangazo ya kibiashara

Hakuna jipya ambalo limetoka kwa sasakatika kikao hiki cha kwanza cha mazungumzo, amearifu mwandishi wetu katika mji wa Brussels, Juliette Gheerbrant. Hata hivyo, shughuli katika makundi madogo zimefanyika kabla ya ufunguzi mkutano huo. Rais wa Ufaransa amekutana na Kansela wa Ujerumani na Waziri Mkuu wa Ugiriki kwa muda wa saa moja Alhamisi asubuhi. "Mjadala wenye lengo la kujenga," wasaidizi wa Rais François Hollande wamebainisha.

Ni wazi kwamba utaratibu wa kuwarejesha wakimbizi nchini Uturuki unapaswa kutekelezwa, itabidi Ugiriki uwezo wa kutosha ili kutathmini ombi la hifadhi la kila mhamiaji. Alexis Tsipras pia amekumbuka wakati alipowawasili katika Baraza la Ulaya kuwa nchi yake inahitaji msaada. Waziri Mkuu wa Ugiriki ameelezea hali inayojiri katika kambi ya wakimbizi ya Idomeni, kwenye mpaka wa kaskazini mwa nchi hiyo, ambapo maelfu ya wahamiaji wameshikiliwa katika hali mbaya kutokana na kufungwa kwa mpaka wa Makedonia. kwa mujibu wa Alexis Tsipras, hali hii ni aibu kwa utamaduni wa Ulaya na itakuwa kuchukua maamuzi kwa ajili ya kutafutia ufumbuzi, kuwasaidi na kuwalindia usalama kwa wakimbizi, lakini pia kuharakisha zoezi la kuwahamisha.

Itakumbuka kwamba, rasimu ya makubaliano na Uturuki inatoa mambo kadhaa:

► kuongeza mara dufu kiasi cha Dola bilioni 3 (ambazo tayari zimetengwa kwaz ajili ya wahamiaji nchini Uturuki)

► Kufuta, kuanzia majira haya, mahitaji ya visa ya muda mfupi kwa raia wa Uturuki wanaoelekea Ulaya

► kubadilishana kati ya mhamiaji na mkimbizi, ikimaanisha mhamiaji alieingia kinyume cha sheria nchini Ugiriki 9 kumrejesha Uturuki) dhidi ya mkimbizi anaeishi nchini Uturuki( kwa kwenda Ulaya)

► kuongeza kasi ya mazungumzo kwa ajili ya kuingizwa kikamilifu kwa Uturuki katika Umoja wa Ulaya.