UBELGIJI-UFARANSA-USALAMA-UGAIDI

Sven Mary, kumfungulia mashitaka mwendesha mashitaka wa Ufaransa

Sven Mary, mwanasheria wa Salah Abdeslam, mbele ya vyombo vya habari, Jumamosi, Machi 19, 2016, alipotoka katika majengo mahakama mjini Brussels.
Sven Mary, mwanasheria wa Salah Abdeslam, mbele ya vyombo vya habari, Jumamosi, Machi 19, 2016, alipotoka katika majengo mahakama mjini Brussels. Aurore Belot / Belga / AFP

Sven Mary, aliechaguliwa na mtuhumiwa muhimu katika mashambulizi ya Paris, Salah Abdeslam, kwa kuhakikisha utetezi wake baada ya kukamatwa kwake Ijumaa, ni mmoja wa wanasheria maarufu wa jinai nchini Ubelgiji, uko tayari kukabiliana na shinikizo kubwa ya vyombo vya sheria vya Ufaransa.

Matangazo ya kibiashara

Sven Mary ametangaza Jumapili hii kwamba atamfungulia mashataka mwendesha mashitaka wa mjini Paris, François Molins, kwa ukiukwaji wa kufichua siri ya kesi ambayo bado inasikilizwa mahakamani.

"kusomwa kwa sehemu ya alivyotamka Bw Abdeslam katika mkutano na waandishi wa habari ni ukiukwaji" wa kufichua siri ya kesi inayosikilizwa mahakamani, amesema Jumapili hii Sven Mary. François Molins alibaini kwamba Abdeslam aliwambia wachunguzi wa Ubelgiji kuwa "alikuwa na mipango wa kujilipua katika uwanja wa mpira wa Ufaransa (Stade de France)" jioni siku hiyo ya mashambulizi lakini baadaye akabadili mawazo yake.

Kwa upande wake mwanasheria Mary, "Salah Abdeslam umuhimu mkubwa kwa uchunguzi huu." "Naweza kusema kuwa ana thamani ya dhahabu. anashirikianai, anawasiliana, hatumii haki yake ya kukaa kimya. Nadhani itakuwa kuniruhusu nizungumze naye, ili wachunguzi waweza kuzungumza naye," amesema Jumapili hii kwenye runinga ya serikali ya RTBF.

Abdeslam alikamatwa nchini Ubelgiji wiki hii miezi minne baada ya kuwa mafichoni.