UBELGIJI-MASHAMBULIZI-UGAIDI

Ubelgiji: Brussels yakumbwa na mashambulizi

Abiria wanaotumia usafiri wa trni za mwendo wa kasi wakiondolewa mjini Brussels, Machi 22, 2016.
Abiria wanaotumia usafiri wa trni za mwendo wa kasi wakiondolewa mjini Brussels, Machi 22, 2016. Reuters

Milipuko miwili imeukumba uwanja wa ndege wa Brussels Jumanne hii asubuhi karibu saa 8:00 saa za Ubelgiji (sawa na 7:00 asubuhi saa za kimataifa). Mwendesha mashitaka wa Ubelgiji amebaini kwamba shambulio hilo ni la "kujitoa mhanga".

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, mlipuko mwingine umetokea katika kituo cha treni za mwendo wa kasi karibu na taasisi za Umoja wa Ulaya. Waziri wa Afya wa Ubelgiji amesema kuwa shambulizi lililotokea katika uwanja wa ndege wa Zaventem mjini Brussel imegharimu maisha ya watu 11 na 81 wamejeruhiwa, wakati ambapo ripoti ya karibuni kutoka shirika la uchukuzi la Brussels limesema watu 15 wamepoteza maisha na 55 kujeruhiwa katika kituo cha treni cha Maelbeek. Waziri Mkuu Charles Michel amelaani mashambulizi hayo akiyataja kuwa ni "mashambulizi ya kijinga, machafu na yasiokuwa na umuhimu wowote."

 ■ Watu wameondolewa katika uwanja wa ndege wa Zaventem mjini Brussels Jumanne hii asubuhi baada ya milipuko kadhaa ilioyakumba majengo ya uwanja huo, karibu saa 8 asubuhi. Uwanja wa ndege umefungwa "hadi itakapotangazwa tena "amri ya kuufungua". maafisa 11 wa zima moto wamesema watu 11 wamepoteza maisha na 81 wamejeruhiwa, taarifa hii imethibitishwa na Waziri wa Afya wa Ubelgiji (RTBF).

■ Mlipuko pia umetokea katika kituo cha treni za mwendo wa kasi karibu na taasisi za Umoja wa Ulaya. Shirika la uchukuzi la Brussels (STIB) limesema shambulio hilo limegharimu maisha ya watu 15 na 55 wamejeruhiwa. Mabasi, treni za mwendo wa kasi na magari mengine vimesimamishwa kufanya kazi.

■ Waziri Mkuu wa Ubelgiji Charles Michel amelihutubia taifa baadae asubuhi.

1:03 mchana : Kwa mujibu wa runinga ya taifa ya Ubelgiji, misako inayohusiana na mashambulizi ya leo asubuhi inaendelea.

12:55 mchana: Kwa mujibu wa taarifa ya ofisi ya mashitaka ya Ubelgiji, milipuko mitatu ya leo asubuhi ni "mashambulizi ya kigaidi." "Kitengo cha kupambana na ugaidi cha Ofisi ya mashitaka ya Ubelgiji kimemkabidhi kesi hii jaji maalum katika masuala ya ugaidi," Ofisi ya mashitaka imesema.

12:45 mchana: Rais wa Ufaransa François Hollande amezungumza mbele ya vyombo vya habari. Ametoa wito kwa "umoja wa kitaifa" dhidi ya tishio la kigaidi. "Vita dhidi ya ugaidi itakuwa ya muda mrefu," pia ameonya.

11:36 mchana Manuel Valls (Waziri Mkuu wa Ufaransa): "Tuko katika vita, tunakabiliwa kwa miezi kadhaa barani Ulaya na vitendo vya vita. Na kutokana na vita hivi, tunapaswa kuhamasisha wakati wote. "

11:34 mchana: Kwa mujibu wa shirika la uchukuzi baina ya wilaya za Brussels (STIB), idadi ya waliopoteza maisha katika kituo cha trni cha Maelbeek imefikia watu 15na 55 wamejeruhiwa, runinga ya serikali (RTBF) imearifu.