POLAND-UBELGIJI-WAKIMBIZI

Mashambulizi Brussels: Poland yakataa kupokea wakimbizi

Beata Szydlo, waziri Mkuu wa Poland.
Beata Szydlo, waziri Mkuu wa Poland. REUTERS/Vincent Kessler

Poland hatimaye imekataa kupokea wahamiaji katika ardhi yake katika mfumo wa mpango wa Umoja wa Ulaya wa kugawana wakimbizi, Waziri Mkuu wa Poland, Beata Szydlo, ametanagaza Jumatano hii, kufuatia mashambulizi ya Brussels.

Matangazo ya kibiashara

"Baada ya kile kilichotokea Jumanne wiki hii mjini Brussels, haiwezekani kwa wakati huu kusema kwamba tuko tayari kukubali kundi lolote la wahamiaji kuingia katika nchi hii," amesema Bi Szydlo kwenye runinga binafsi ya Superstacja. Hadi sasa, serikali yake imekua imekubali kupokea wakimbizi 7,000, kwa kuheshimu ahadi iliyotolewa na serikali iliyopita ya Ewa Kopacz.

Poland ni ya nchi ya kwanzaUmoja wa Ulaya kuchukua uamuzi huo baada ya mashambulizi ya mjini Brussels yaliogharimu maisha ya watu 31 na 270 kujeruhiwa. Raia watatu kutoka Poland ni miongoni mwa watu waliojeruhiwa katika mashambulizi hayo.

"Tunalazimika kwanza kuweka mbele suala la usalama wa wananchi wetu," ameongeza Bi Szydlo, akitoa wito kwa Ulaya kukataa kuwa mwenyeji wa "maelfu ya wahamiaji wanaokuja hapa tu kuboresha hali yao ya maisha."

Miongoni mwa wahamiaji hawa, "pia kuna magaidi," Bi Szydlo amesema.

wakimbizi wa kwanza wangeliwasili nchini Poland mwishoni mwa mwezi Machi au mapema mwezi Aprili.

Bi Szydlo ametetea nafasi "iliyo makini" ya nchi za Visegrad(Hungary, Poland, Jamhuri ya Czech na Slovakia), Romania na Croatia dhidi ya baadhi ya nchi kukubali kutekeleza mpango wa Umoja wa Ulaya, ikiwa ni pamoja na Ujerumani, katika mapokezi ya wahamiaji.