UBELGIJI-UFARANSA-USALAMA-UGAIDI

Mashambulizi ya Paris: Salah Abdeslam aomba kurudishwa Ufaransa

Sven Mary, mwanasheria wa Salah Abdeslam, Machi 24, 2016.
Sven Mary, mwanasheria wa Salah Abdeslam, Machi 24, 2016. DIRK WAEM / Belga / AFP

Mtuhumiwa mkuu wa mashambulizi ya mjini Paris, Salah Abdeslam, baada ya kukamatwa Ijumaa Machi 18, sasa ameanza kuomba kusafirishwa Ufaransa ili aweze kujieleza kuhusu tuhuma dhidi yake.

Matangazo ya kibiashara

Salah Abdeslam alikua ameanza kushirikiana vema na mamlaka ya Ubelgiji, lakini tangu Machi 22, siku ya mashambulizi ya mjini Brussels alikataa kushirikiana na wachunguzi na kukana kuwa hana uhusianowowote na mashambulizi ya mjini Brussels. Kwa mujibu wa mwanasheria wake, ameomba arejeshwe nchini Ufaransa ili aweze kujieleza..

Salah Abdeslam anataka kuondoka Ubelgiji haraka iwezekanavyo ili aweze kusafiri kwenda Ufaransa. Maneno haya yamethibitishwa na mwanasheria wake alipokua akitoka katika kikao kifupi mapema asubuhi mbele ya majaji wa Mahakama. Uamuzi huo umekaribishwa na mwanasheria wa Salah Abdeslam, Sven Mary: "Ameelewa kwamba kwa kweli kesi hapa ... ni mfano wake tu ... Hivyo nadhani anataka kujieleza nchini Ufaransa ... ni jambo jema. "

Kikao cha Alhamisi hii asubuhi kilikua kinahusu uamuzi uliochukuliwa na majaji dhidi ya Salaha Abdeslam wa kuendelea kusikiliwa kwake. Hata hivyo kikao hicho kimeahirishwa kwa ombi la mwendesha mashitaka wa Abdeslam. Mambo yanapaswa kwenda haraka, amebaini Sven Mary, mwanasheria wa kijana huyo Mfaransa mwenye asili ya Morocco: "Mimi ntamuona jaji alie na kesi hii mikononi, ili asiwezi kupinga safari hii na kutumwa kwa mteja wangu nchni Ufaransa, zoezi ambalo linaweza kufanyika, natarajia (...) haraka iwezekanavyo. Nadhani ni suala kweli la wiki moja tu. Machi 31 atasikilizwa kwa kutekeleza hati ya kukamatwa ya Ulaya na nadhani kwamba baada ya Machi 31(...) hakutakuwa na rufaa yoyote, wala kupinga. Hivyo tutafuata nia yake na ni jambo zuri sana. "

Licha ya kuwa anatuhumiwa kuwa mmoja wa waandaaji wa mashambulizi ya Novemba 13 mjini Paris, Abdeslam anasadikiwa kuwa alikua akiwasiliana na walipuaji waliojitoa mhanga Jumanne Machi 22 mjini Brussels. Kwa hali hii, mwanasheria wake amesema kuwa Salah Abdeslam hana uhusiano wowote wa kile kilichotokea katika mji mkuu wa Ubelgiji.