UBELGIJI-MASHAMBULIZI-UGAIDI

Watuhumiwa 3 washtakiwa kwa kosa la ugaidi Ubelgiji

Askari polisi wakito ulinzi mbele ya kituo cha treni baada ya mashambulizi yalioukumba mji mkuu wa Ubelgiji, tarehe 22 Machi.
Askari polisi wakito ulinzi mbele ya kituo cha treni baada ya mashambulizi yalioukumba mji mkuu wa Ubelgiji, tarehe 22 Machi. REUTERS/Christian Hartmann

Ofisi ya mashitaka ya Ubelgiji imetangaza Jumamosi hii Machi 26 kuwa imewafungulia mashitaka watu watatu. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Ubelgiji, mmoja wao, Faisal C. anaweza kuwa gaidi watatu aliekuwepo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mjini Brussels Machi 22.

Matangazo ya kibiashara

Faisal C, anaedaiwa kama "mtu aliekuwa akivaa kofia" akionekana kwenye picha ya video za ulinzi za CCTV sambamba na walipuaji wawiliwaliojitoa mhanga.

Faisal C., aliekamatwa Alhamisi, Machi 24, ameshtakiwa kwa kosa la "mauaji ya kigaidi" na "kushiriki katika kundi la kigaidi", Ofisi ya mashitaka ya Ubelgiji imetangazaJumamosi hii. Hakuna silaha au vilipuzi viliokamatwa wakati wa operesheni ya msako iliyoendeshwa nyumbani kwa mtuhumiwa huyo, Ofisi ya mashitaka imebaini.

Watu wengine wawili wameshtakiwa pia kwa shughuli za kigaidi na kujiunga na kundi la kigaidi. Mmoja wao anatambuliwa kama Abubakar A. Mtuhumiwa mwingine, ni Rabah N., alikuwa anatafutwa kuhusiana katika operesheni ilioendeshwa wiki hii nchini Ufaransa, ambayo kwa mujibu wa mamlaka imesaidia kuzuia shambulio.

Vyombo vya habari vya Ubelgiji vinabaini kwamba Faisal C., anaweza kuwa "mtu aliekuwa akivalia kofia," ambaye alionekana kwenye picha ya kamera za ulinzi za CCTV akiwa amesimama pamoja na walipuaji wawili waliojitoa mhanaga katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zaventem mjini Brussels, Ibrahim El Bakraoui na Najim Laachraoui. Taarifa ambayo Ofisi ya mashitaka ya Ubelgiji haijathibitisha.

Picha iliyopigwa na kamera ya ulinzi kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zeventem mjini Brussels ikionysha watuhumiwa wa mashambulizi yaliotokea mjini humo, Machi 22.
Picha iliyopigwa na kamera ya ulinzi kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zeventem mjini Brussels ikionysha watuhumiwa wa mashambulizi yaliotokea mjini humo, Machi 22. REUTERS/CCTV/Handout via Reuters

Tangu Alhamisi, watu tisa katika kwa jumla wamekamatwa nchini Ubelgiji na wawili nchini Ujerumani baada ya mashambuliziyaliogharimu maisha ya watu 31 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zaventem na katika kituo cha treni za mwendo wa kasi cha Maelbeek mjini Brussels, Machi 22.