UBELGIJI-MISAKO-UGAIDI

Ubelgiji: watuhumiwa waendelea kukamatwa

Askari polisi wa Ubelgiji wakitoa ulinzi katika eneo lililo karibu na jengo la mahakama mjini Brussels, 24 mars.
Askari polisi wa Ubelgiji wakitoa ulinzi katika eneo lililo karibu na jengo la mahakama mjini Brussels, 24 mars. REUTERS/Christian Hartmann

Ofisi ya mashitaka ya Ubelgiji imetangaza kuwa watu wanne wamewekwa chini ya ulinzi Jumapili hii Machi 27 kufuatia zoezi la misako kumi na tatu dhidi ya ugaidi katika miji kadhaa nchini Ubelgiji, siku tano baada ya mashambulizi ya mjini Brussels.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo, vyombo vy sheria vya Ubelgiji vimemfungulia mashitaka mtuhumiwa wa pili katika uchunguzi kuhusu mpango wa shambulio uliyotibuliwa nchini Ufaransa Alhamisi Machi 24.

Misako minne imeendeshwa Jumapili asubuhi katika miji ya Malines na Duffel, miji miwili ya jimbo llinalokaliwa na watu kutoka jamii ya Flanders, kaskazini mwa nchi. Misako mingine minane ilifanyika katika maeneo mablimbali ya mji wa Brussels.

"Kwa ujumla, watu tisa wamepelekwa kusikilizwa" katika "kesi ya ugaidi" lakini "watano kati yao waliachiliwa," Ofisi ya mashitaka imesema katika taarifa yake. Ofisi ya Mashitaka, hata hivyo, haiko weka bayana kama operesheni hizo zilikua zinahusiana na uchunguzi kuhusu mashambulizi ya mjini Brussels yaliogharimu maisha ya watu 31 Machi 22.

"Hakimu anaechunguza kesi hiyo anatazamiwa kuamua baadaye Jumapili hii mchana," kuendelea kuwashikilia watu hao wanne waliosikilizwa au la," Ofisi ya mashitaka imeongeza, huku ikikataa kutoa matokeo ya zoezi la misako.

Mtuhumiwa wa pili ashtakiwa katika uchunguzi wa shambulizi lililotibuliwa Ufaransa

Wakati huo huo, mtuhumiwa wa pili amefunguliwa mashitaka nchini Ubelgiji katika uchunguzi wa mpango wa shambulizi lililotibuliwa nchini Ufaransa Alhamisi Machi 24. Mashitaka ya Abderamane Ameuroud ya "kushiriki katika kundi la kigaidi" yanajiongeza katika kesi hii mpya kati ya Ufaransa na Ubelgiji, na ile ya Rabah N.

Abderahmane Ameuroud alijeruhiwa kwenye mguu na kukamatwa wakati wa operesheni kubwa ya kupambana dhidi ya ugaidi katika mtaa wa Schaerbeek Ijumaa Machi 25. Raia huyo wa Algeria, mwenye umri wa miaka arobaini si mgeni katika Idara ya Ujasusi ya Ufaransa.

Abderahmane Ameuroud tayari amekwisha hukumiwa Mei 2005 na Mahakama ya Paris kwa kifungo cha miaka 7 jela na kupigwa marifukukuingia katika ardhi ya Ufaransa, kutokana na kosa la kushiriki katika mauaji ya Massoud, mkuu wa majeshi ya Afghanistan. Alihukumiwa baada ya kupatikana na hatia ya kutoa msaada wa vifaa kwa raia wawili wa Tunisia waliomuua kiongozi wa upinzani dhidi ya Taliban mwezi Septemba 2001, katika usiku wa mashambulizi ya Septemba 11 nchini Marekani.

Abderahmane Ameuroud pia anatuhumiwa kuwa aliwasajili nchini Ufaransa wapiganaji wa kijihadi na kupanga mafunzo katika msitu wa Fontainebleau, katika jimbo la Seine-et-Marne, mwandishi wetu nchini Ubelgiji, Laxmi Lota, amearifu.