UBELGIJI-SHAMBULIO-USALAMA-SHERIA

Mashambulizi Brussels: Faisal Cheffou aachiliwa

Video iliyorushwa kwenye YouTube mwaka  2014 ikimuonyesha Faisal Cheffou, akijitambulisha kama mwandishi wa habari binafsi, alishtakiwa katika uchunguzi kuhusu mashambulizi ya Brussels.
Video iliyorushwa kwenye YouTube mwaka 2014 ikimuonyesha Faisal Cheffou, akijitambulisha kama mwandishi wa habari binafsi, alishtakiwa katika uchunguzi kuhusu mashambulizi ya Brussels. AFP

Faisal Cheffou, aliyeshtakiwa katika uchunguzi wa mashambulizi ya mjini Brussels na kutuhumiwa awali kuwa mtu watatu aliyehusika katika shambulizi lililotokea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zaventem, ameachiliwa huru, Ofisi ya mashitaka ya Ubelgiji imetangaza Jumatatu hii.

Matangazo ya kibiashara

"Dalili zilizopelekea kukamatwa Faisal Cheffou hazikwenda na uchunguzi unaoendelea mpaka sasa. Kutokana na hali hiyo, mtuhumiwa huyo ameachiliwa huru na afisaa wa mashitaka," Ofisi ya mashitaka imesema katika taarifa yake bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi.

Ofisi ya mashitaka ya Ubelgiji ilitangaza Jumamosi Machi 26 kuwa iliwafungulia mashitaka watu watatu. Vyombo vya habari vya Ubelgiji, vilibaini kwamba Faisal C. ni mmoja wa watuhumiwa hao waliofunguliwa mashitaka na ambaye anaweza kuwa gaidi watatu aliekuwepo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mjini Brussels Machi 22.

Faisal C, anaedaiwa kama "mtu aliekuwa akivaa kofia" akionekana kwenye picha ya video za ulinzi za CCTV sambamba na walipuaji wawili waliojitoa mhanga.
Faisal C., aliekamatwa Alhamisi, Machi 24, alikua ameshtakiwa kwa kosa la "mauaji ya kigaidi" na "kushiriki katika kundi la kigaidi". Hakuna silaha au vilipuzi viliokamatwa wakati wa operesheni ya msako iliyoendeshwa nyumbani kwa mtuhumiwa huyo, Ofisi ya mashitaka ilibaini.

Watu wengine wawili walishtakiwa pia kwa shughuli za kigaidi na kujiunga na kundi la kigaidi. Mmoja wao anatambuliwa kama Abubakar A. Mtuhumiwa mwingine, ni Rabah N., alikuwa anatafutwa kuhusiana katika operesheni ilioendeshwa wiki iliyopita nchini Ufaransa, ambayo kwa mujibu wa mamlaka imesaidia kuzuia shambulio.

Vyombo vya habari vya Ubelgiji vilieleza kwamba Faisal C., anaweza kuwa "mtu aliekuwa akivalia kofia," ambaye alionekana kwenye picha ya kamera za ulinzi za CCTV akiwa amesimama pamoja na walipuaji wawili waliojitoa mhanaga katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zaventem mjini Brussels, Ibrahim El Bakraoui na Najim Laachraoui. Taarifa ambayo Ofisi ya mashitaka ya Ubelgiji haijathibitisha.

Jumapili, mwishoni mwa jumalililopita Ofisi ya mashitaka ya Ubelgiji imlitangaza kuwa watu wanne wamewekwa chini ya ulinzi kufuatia zoezi la misako kumi na tatu dhidi ya ugaidi katika miji kadhaa nchini Ubelgiji, siku tano baada ya mashambulizi ya mjini Brussels.