MAREKANI-ULAYA YA MASHARIKI-USALAMA

Pentagon kutuma kikosi cha kudumu Ulaya ya Mashariki

Kifaru cha jeshi la Marekani kiitwacho Abrams kiliotumwa katika mji wa Riga, Latvia, Machi 9, 2015
Kifaru cha jeshi la Marekani kiitwacho Abrams kiliotumwa katika mji wa Riga, Latvia, Machi 9, 2015 AFP

Marekani inapania kutuma kikosi cha wanajeshi wa kudumu watakaokua wakibadilishwa kila mara katika Ulaya ya Mashariki ifikapo Februari 2017, kama sehemu ya jitihada zake za kuzuia uwezekano wa uchokozi kutoka Urusi, Pentagon imesema Jumatano hii.

Matangazo ya kibiashara

"Askari wa kikosi hiki watakua wanabadilishwa kila mara, hivo kuruhusu uwepo wa kikosi cha kudumu chenye magari ya kivita na mafunzo yataboreshwa huku kukiwa na mazoezi pamoja na washirika " wa NATO, amesema Laura Seal, msemaji wa Pentagon.

Kutakuwa na "uwepo endelevu wa kikosi cha kudumu Ulaya ya Mashariki," Seal amebaini.

Pentagon na NATO walikua tayari wamejadili kupelekwa kikosi cha askari watakaokua wakibadilishwa kila mara katika Ulaya ya Mashariki, bila hata hivo kutoa ratiba iliyo wazi.

Mwezi Februari Washington ilitangaza nia yake ya kuongeza mara nne mwaka 2017, gharama zake hadi kufikia Dola bilioni 3.4 zitakazotumiwa kwa kuimarisha jeshi la Marekani barani Ulaya.

Pamoja na kikosi hiki chenye askari 4,200 ambao watakua na vifaa vya kivita ikiwa ni pamoja na vifaru na magari ya kivita), kitakuwa na vitengo vitatu vya kivita barani Ulaya.

Pamoja na vitengo vyote, jeshi la Marekani lina askari 62,000 barani Ulaya.

Moscow imekua ikionya mara kwa mara dhidi ya "uwepo wa askari wa kudumu" kutoa nchi washirika katika mpaka wake, ambapo inaona kuwa ni kinyume na sheria inayounda NATO-Urusi , iliyosainiwa mwaka 1997.