UBELGIJI-HAKI

Hali ya "kutovumiliwa" yashuhudiwa katika magereza Ubelgiji

Katika gereza la mjini Brussels la Forest, "hali imekua ya sintofahamu" wakati ambapo askari magereza kusini mwa Ubelgiji wanaingia wiki yao ya tatu ya mgomo. Mgomo ambao umepelekea serikali kushindwa kupatia ufumbuzi madai ya askari hao magereza licha ya kukosolewa vikali.

Gereza la Forest, Brussels, wakati wa mgomo wa askari magereza, Februari 7, 2013.
Gereza la Forest, Brussels, wakati wa mgomo wa askari magereza, Februari 7, 2013. AFP
Matangazo ya kibiashara

"Hali imezidi kuwa mbaya katika baadhi ya magereza ya Ubelgiji, na kuna hali ya sintofahamu ndani ya gereza," mkurugenzi wa gereza la Forest, Vincent Spronck, amewaambia waandishi wa habari Jumanne hii asubuhi. "Mahabusu hawaruhusiwa kuonana na ndugu zao, wote wamesalia ndamni ya vyomba vyao, hawapumui na hawabadili nguo. Hali sio nzuri kwa kweli! Ni lazima kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huu," Vincent Spronck amenung'unika.

Katika siku za karibuni, matukio mbalimbali yalizuka katika magereza 17 yanayoendelea kuathirika na mgomo huo wa maofisa wa magereza ya Wallonia na Brussels dhidi ya kupunguzwa kwa wafanyakazi na "posho" ya kwa watumishi.

Mapambano baina ya mahabusu yamekithiri kutokana na kunyimwa ruhusa ya kuonana na ndugu au jamaa zao, vifaa kadhaa vimekua vikivunjwa, na vingine kuchomwa moto ... Katika baadhi ya magereza, "Hali inatisha" amehakikisha mwanasheria Alexis Deswaef, kiongozi wa shirika la Haki za Binadamu, ambaye amelaani "mazingira ya kuzuiliwa" akibaini kwamba "wafungwa wanafungwa kama wanyama."

Mgomo unaendelea na Makubaliano ya itifaki kati ya Waziri wa Sheria, Koen Geens, na vyama vya maofisa wa magereza yalitupiliwa mbali mwishoni mwa wiki iliyopita.

Tangu wakati huo, mazungumzo hayo yameshindikana: Bw Geens amehakikisha kwamba "alizidi kiwango cha bajeti kilichowekwa na serikali" katika makubaliano na maofisa wanaogoma, na jeshi ilibidi liombwe kutoa "msaada wa kibinadamu" kwa wafungwa.

Hadi sasa, askari zaidi ya kumi peke ndio ambao wametumwa katika magereza 3 kwa jumla ya 17 yanayoathirika katika mji wa Lantin (mashariki mwa Ubelgiji), pamoja na katika yale ya Forest na Saint-Gilles,katika viunga vya Brussels.