UTURUKI-SHAMBULIO

Watu 3 wauawa, zaidi ya 45 kujeruhiwa Diyarbakir

Askari polisi wa Uturuki akiwa katika eneo la tukio, baada ya shambulio lililogharimu maisha ya watu 3, Mei 10, 2016 Diyarbakir
Askari polisi wa Uturuki akiwa katika eneo la tukio, baada ya shambulio lililogharimu maisha ya watu 3, Mei 10, 2016 Diyarbakir AFP

Watu 3 wameuawa na engine 22 kujeruhiwa Jumanne hii katika mlipuko wa bomu lililotegwa ndani ya gari wakati gari la polisi lilipokua likipita katika mji wa Diyarbakir, mji mkuu wa kusini mashariki wenye wakazi wengi kutoka jamii ya Wakurdi wa Uturuki, shirika la habari la Anatolia linalounga mkono serikali limearifu.

Matangazo ya kibiashara

Vyombo vya habari vya Uturuki vimelihusisha kundi la waasi la PKK katika shambulio hilo.

Katika majira ya joto mwaka uliyopita, kundi la waasi la PKK lilianzisha upya mapambano yake ya kijeshi dhidi ya vikosi vya usalama vya Uturuki baada ya miaka miwili ya mkataba wa usitishwaji mapigano

Siku za hivi karibuni Uturuki imeshuhudia visa vya mashambulizi ambayo vimegharimu maisha ya watu kadhaa nchini humo.