UTURUKI-IS

Uturuki yawashikilia wapiganaji wa IS

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan. REUTERS/Kayhan Ozer/Presidential Palace Press Office/Handout via

Uturuki inasema maafisa wake wa usalama, wanawashikilia wapiganaji saba wa Islamic State akiwemo mmoja wa Makanda wao ambaye amekuwa akitekeleza mauaji.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema wafuasi hao wa Islamic State walikamatwa na kuzuiliwa baada ya uvamizi wa wanajeshi wa Uturuki katika eno la Elazig Mashariki mwa nchi hiyo.

Muuaji anayezuiliwa amefahamika tu kama F.S na inadaiwa amekuwa akitekeleza mauaji ya watu nchini Syria kwa niaba ya Islamic State.

Vyombo vya Habari nchini Uturuki vinaripoti kuwa, wafuasi hao wa IS walikuwa wamekwenda Mashariki mwa nchi hiyo kuwatafuta wanachama wapya kuugana nao.

Uturuki imekuwa ikiyashtumu mataifa ya Magharibi kwa kutofanya jitihada za kutosha kupambana na Islamic State nchini Iarq na Syria.

Mashambulizi kadhaa yamekuwa yakiripotiwa nchini Uturuki katika siku za hivi karibuni na kuilazimu serikali kutuma wanajeshi mipakani ili kupamabana na wanajihadi hao wa Islamic State.