UFARANSA-MAANDAMANO

Maandamano ya polisi dhidi ya "chuki"

Askari polisi wametolewa wito wa kuandamana Jumatano hii saa sita mchana nchini Ufaransa kwa kukemea "chuki dhidi ya unyanyasaji", maandamano ya kwanza baada ya miezi miwili ya makabiliano wakati mwingine yenye vurugu katika maandamano ya uhamasishaji dhidi ya sheria ya ajira.

Polisi ya Ufaransa ikijaribu kuutawanya umati wa watu wanaoandamana dhidi ya sheria ya ajira katika eneo muhimu la Jamhuri, Paris, Machi 31, 2016.
Polisi ya Ufaransa ikijaribu kuutawanya umati wa watu wanaoandamana dhidi ya sheria ya ajira katika eneo muhimu la Jamhuri, Paris, Machi 31, 2016. THOMAS SAMSON / AFP
Matangazo ya kibiashara

Vyama vikuu vya polisi vimewatolea wito askari polisi, waliostaafu na wale waliorejeshwa katika masha ya kiraia, kukusanyika katika miji sitini. Mkusanyiko mkubwa unatazamiwa kufanyika katika eneo muhimu la Jamhuri mjini Paris, ambapo kunakusanyika kila jioni raia makundi ya wanaharakati na vijana tangu Machi 31.

Ishara ya mvutano kwa sasa, miungano ya mashirika na asasi mbali wanoalaani machafuko yanayosababishwa na polisi pia wameto wito kwa raia kufanya maandamano katika eneo hilo muhimu la mji mkuu, kabla ya mkusanyiko wa vyama vya polisi.

Vyama hivi vinabaini kwamba vinaitikia wito wa wenzao wanaoendesha kazi yao katika kuimarisha usalama tangu maandamano kuanza, wakati ambapo zaidi ya askari 350 wamejeruhiwa mpaka sasa, kwa mujibu wa viongozi. Kumi na moja miongoni mwao wamejeruhiwa katika makabiliano ya jana Jumanne, Wizara ya Mambo ya Ndani imesema.

Mashirika mengi ya haki za binadamu yamenyooshea kidole cha lawama askari polisi kwamba wao ndio wanahusika na vurugu. Hata hivyo waandamanji wamekua wakiamba kila mara kwamba "kila mtu anachukia polisi". Hivi karibuni kijana mmoja alipoteza jicho lake moja baada ya kupigwa na polisi mwishoni mwa mwezi Aprili katika mji wa Rennes. Uchunguzi wa "Polisi" (IGPN) kuhusu madai ya ukatili wa polisi umefunguliwa nchini Ufaransa, na wanasiasa wengi kutoka mrengo wa kushoto pamoja na vyama vya wafanyakazi wameishtumu serikali kujihusisha na vurugu katika kuimarisha usalama.